Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
JAMII imeaswa kujenga utamaduni wa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo watu wenye mahitaji ya viungo bandia kutokana na gharama ya upatikanaji wa viungo hivyo na wenye uhitaji kushindwa kumudu gharama.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya LALJI foundation, Fatma Mussa wakati akikabidhi msaada wa viungo bandia kwa wagonjwa 11 katika Hospitali ya CCRBT Dar es salaam leo Jumatano Desemba 18, 2024.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo amesema lengo ni kugusa watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii ambapo pia amewataka wadau na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi hizo.
Hii ni mara ya tatu kwa taasisi ya LALJI foundation kutoa msaada kwa wagonjwa wenye uhitaji wa viungo bandia hospitali ya CCBRT ikiwa ni utamaduni wa taasisi hiyo kusaidia watu wenye uhitaji.
More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi