Zaidi ya wananchi 2000 wa Songea Vijijini Mkoani Ruvuma wanatarajiwa kunufaika na huduma ya kambi ya matibabu ya macho bure inayoendeshwa na taasisi ya LALJI FOUNDATION kwa kushirikiana na Rotary Club Masaki na Lions Club District 411C ikiwa ni muendelezo wa taasisi hiyo kusaidia watu wenye matatizo ya macho.
Kambi hiyo ya siku nne inatarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 2000 ambao wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya macho huku watu 100 wakitarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mtoto wa jicho baada ya kugundulika kuwa na tatizo hilo wakati wanafanyiwa uchunguzi.
Akizungumza wakati wa kambi hiyo Mwenyekiti wa taasisi ya LALJI FOUNDATION Ndugu Imtiaz Lalji amesema taasisi hiyo itaendelea kuweka kambi ya macho mkoani Ruvuma kwasababu muitikio na uhitaji wa watu ni mkubwa hivyo zoezi hilo litakua endelevu ili kuwafikia watu wengi zaidi.
Amesema ” watu wa Ruvuma wachangamkie fursa ya kambi hiyo kwa kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma ya uchunguzi na matibabu ya macho bure “.
Baadhi ya wananchi walionufaika na huduma hiyo wameishukuru taasisi ya LALJI FOUNDATION kwa kufanikisha zoezi hilo huku wakitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitoa kusaidia watu wenye uhitaji.
More Stories
TMA :Mvua za masika kuanza mwanzoni mwa mwezi Machi
Maandamano ya kuunga mkono Samia, Mwinyi yatikisa Tabora
Haya hapa matokeo yote kabisa ya Form Four