December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KWA TAARIFA YAKO: Watu milioni 50 Duniani wamelewa pombe wakati wote

Na Mwandishi Wetu

WATU milioni 50 Ulimwenguni (sawa na asilimia 0.7 ya watu wote duniani) wamelewa pombe muda huu wakati unaposoma taarifa hii.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), pamoja na kwamba Bara Ulaya ndio linaongoza kwa unywaji pombe zaidi, Bara la Afrika ndilo lenye mzigo mkubwa zaidi wa madhara yanayotokana na unywaji pombe kama vile vifo, majeraha na athari nyingine zizokanazo na ajali za barabarani.

Hata hivyo ripoti hiyo inayotolewa WHO kila mwaka ijulikanayo kama Ripoti ya Hali ya Kiafya na Unywaji Pombe Duniani (Global Status Report on Alcohol and Health) inaeleza kwamba asilimia 45 ya watu Ulimwenguni hawajawahi kunywa pombe, ambapo asilimia 35 ni wanaume na wanawame ni asilimia 55.

Kwa maana hiyo ni kwamba nusu ya wanaume na theluthi mbili ya wanawake wote duniani wameweza kujizuia na unywaji pombe kwa mwaka (miezi 12). Tafakari, wewe na mimi upo kwenye kundi lipi kati ya wanaokunywa pombe na wasiokunywa?