November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kuzimwa mtambo Ruvu chini kwa saa 36

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam( DAWASA) inawatangazia wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini uliopo wilayani Bagamoyo, kuwa mtambo utazimwa kwa saa 36 siku ya Jumatatu tarehe 30/1/2023.

Lengo ni kuruhusu kufanyika kazi ya kusafisha mifumo yote ya mtambo ikiwemo machujio, matanki yote ya maji na mabomba makuu yote ya kusafirisha maji kutoka katika mtambo huo.

Kutokana na kazi hiyo, maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo yatakosa huduma ya maji kuanzia Jumatatu asubuhi hadi Jumanne jioni; Maeneo hayo ni Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Zinga, Kerege, Mabwepande, Bunju, Kunduchi, Mbezi Beach, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang’ombe, Keko, Kurasini, Uwanja wa ndege, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya mji.Mamlaka inawaomba Wananchi kukumbuka kuhifadhi maji ya kutosha ili kuweza kuyatumia kipindi chote cha matengenezo.

DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.