December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Daktari: kuna uhitaji mkubwa upandikizaji figo nchini

Na   Aveline  Kitomary, TimesMajira Online, Dar es Salaam

RAIS wa Chama cha Wataalamu wa Figo Tanzania, Dk Onesmo Kisanga, amesema kunauhitaji mkubwa wa upandikizaji figo nchini huku kukiwa na changamoto kadhaa.

Akizungumza na Gazeti la MAJIRA katika mahojiano maalum,Dk Kisanga ambaye pia ni  Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili(MNH),  amesema zaidi ya wagonjwa wa figo 1,000 nchini kote wanahitaji huduma lakini wanakosa kutokana na upatikanaji mgumu wa figo.

Dk Kisanga amebainisha kuwa ugonjwa wa figo uko kwa asilimia 10 kwa ukanda wa jangwa la Sahara  huku utafiti wa ngazi ya jamii  uliofanywa kaskazini mwa nchi kwa Mkoa wa Kilimanjaro ukionesha asilimia 6.7 ya watu wanatatizo la figo sababu ikiwa ni ukosefu wa elimu.

“Uhitaji wa upandikizaji wa figo ni mkubwa kuna wagonjwa 1,000 wanaosafishwa figo hawa pia wanahitaji kupandikizwa ,tangu huduma hii ya upandikizaji ianze tumepandikiza watu 62 ndani ya nchini.

“Changamoto ni kupata watu wanatoa figo hapa panakuwa pagumu kwasababu  ni lazima figo inayotolewa  iwe salama na mnakubaliana na kuna vipimo ambayo vinayoendana na mgonjwa wakati mwingine ndugu  anaweza kupatikana lakini vipimo vikifanyia haendani na mgonjwa.

Dk Kisanga amesema kuwa matibabu ya figo ni gharama hali inasababisha umasikini katika familia za wahusika.

“Hatua ya kwanza na tatu inaweza kutibika ila ya nne na tano inakuwa ngumu ni kusafisha damu na kupandikiza figo

“Kwa hatua hizo za  kubadilisha damu gharama ni Sh milioni tatu  hadi nne kwa mwezi mmoja  na  kila mwezi lazima asafishe ,upande wa Upandikizaji ni Sh milioni 20,”ameleza Dk Kisanga.

Amesema kuwa sababu zinazochangia magonjwa ya figo ni magonjwa sugu kama kisukari,magonjwa ya presha,magonjwa ya mfumo wa mkojo ,magonjwa kurithi na mengine.

“Kuna magonjwa ya figo ya ghafla  kama akinamama wakati wa uzazi na ajali  hapa damu nyingi ikpotea anapata ugonjwa lakini akiongezewa anapata nafuu,Kuumwa na nyoka,nyuki na dawa za kulevya,”amebainisha. 

Dk Kisanga amesema katika kuadhimisha siku ya figo wanatoa elimu kwa jamii ili waweze kuelewa ugonjwa huo.

“Pamoja na figo kuumwa lakini lazima maisha yaende tunaelimisha na tunajitahidi kuzuia na hata kama kuna mgonjwa tunahakikisha yanaendelea vizuri.

“Kazi ya figo kuchuja maji yasiyohitaji na vinatoka nje kwa njia ya mkonjo.kuimarisha mifupa,kuweka kiwango cha damu kizuri ,mifumo ya mwili kukaa sawa.

Ametoa ushauri kwa jamii kuchunguza afya ili kubaini tatizo mapema na kupata matibabu ya haraka.

“Kuna vituo vya afya nchini unaweza kupata matibabu ya figo,tunasisitiza kuwahi kwenda kwenye vituo vya tiba  vitu kama uzito ukizidi unaweza kuharibu figo ,lishe kwa kiasi ,watu wafanye mazoezi na kuzingatia mtindo bora wa maisha.

“Na pia ni muhimu kuwa na kadi ya bima ya afya  kwani inasaidia kumudu gharama za matibabu na kuondoa mzigo wa fedha zinazotakiwa wakati wa matibabu nasisitiza kukata kadi ya bima ni muhimu zaidi,”amesisitiza Dk Kisanga.