Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
MWAKA huu (2022) ambao unaelekea ukingoni umekuwa ni faraja kubwa kwa wazazi na wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia zenye kipato duni baada ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kufuta ada kidato cha tano na sita.
Uamuzi wa elimu bure hadi ulifikiwa Juni, mwaka huu baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Mwigulu Nchemba kuwasilisha mapendekeza Bungeni ya kufutwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita ili kuwapunguzia gharama.
Mwigulu aliwasilisha mapendekezo hayo Juni 14, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.
Dkt. Mwigulu alisema kwa kwa wakati huo wanafunzi wa kidato cha tano ni takribani 90,825 na kidato cha sita ni 56,880 na mahitaji ya fedha ni sh. bilioni 10. 3 bilioni.
Wakizungumza na Majira kuhusiana na mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwaka huu, wananchi wengi wamesema ni pamoja na kufuta ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Mwalimu John Samwel, alisema kati ya mambo makubwa ambayo Rais Samia amefanya katika sekta ya elimu kwa mwaka huu ni pamoja na kufuta ada ya kidato cha tano na sita.
Alisema ada hiyo ilikuwa kikwazo kwa watoto wengi ambapo baadhi walishindwa kufikia ndoto zao kwa wazazi kushindwa kumudu ada hiyo. “Mimi nimekuwa mwalimu kwa muda mrefu.
Ada ya sh. 70,000 waliyokuwa wakilipa wanafunzi wa kidato cha tano na sita kuna watu wanaona ni ndogo, lakini ni kubwa, kwani wengi walikuwa wanashindwa kuilipa.
“Kwa hiyo uamuzi wa Rais Samia kufuta ada hii amegusa maisha ya walalahoi wengi, ninaamini kila mtoto atafikia ndoto yake. Hakuna kitu kilichokuwa kinaniumiza katika maisha yangu kuona mtoto anaacha masoko kwa kushindwa kulipa ada,” anasema Samwel.
Naye Egdar Swai, alisema Sera ya elimu bila malipo ilianza chini ya serikali ya awamu ya tano mwaka 2015.
Alisema Sera hii inamaanisha kufutwa kwa ada zote katika shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na michango ya wazazi katika ngazi ya elimu ya msingi.
Kwa mujibu wa Swai, kufutwa kwa ada hiyo kulitokana na tamko lililotolewa na Waziri wa TAMISEMI kwa wakati ule, George Simbachawene. “Lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani alienda mbali zaidi na kuamua kufuta ada ya kidato cha tano na sita.
Uamuzi huu umeleta ahueni kubwa kwa wazazi/walezi hasa kulingana na hali duni za kiuchumi za Watanzania walio wengi. Hatua hii imeleta tija kubwa katika sekta ya elimu nchini kwani inatoa fursa kwa kila Mtanzania kupata elimu ya sekondari ya juu,” anasema Swai.
Pamoja na uamuzi huo kuleta faida kubwa kwa wazazi, anasema umepeleka mzigo mkubwa kwa wakuu wa shule pamoja na wenyeviti wa kamati za shule kwani wazazi wengi wanadhani jukumu la kupata elimu kwa watoto wao ni la Serikali peke yake.
“Nadhani wazazi/walezi wengi wamechagizwa na maneno ya wanasiasa majukwaani na kusahau suala la kupata elimu iliyobora ni jukumu na ushirikiano wa pamoja kati ya serikali, wazazi/walezi na wanafunzi.
Upande wa serikali unafanya vyema kutimiza wajibu wake toka sera hii ianzishwe rasmi mwaka 2016. Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa elimu bila malipo,” anasema Swai.
Naye Dawson Petrol anasema kufutwa kwa ada hiyo muendelezo wa mambo mbalimbali makubwa yanayoendelea kufanywa chini ya uongozi wa Rais tangu aapishwe kwa mujibu wa katiba kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huo.
Alisema Watanzania wenye kipato cha chini hawana cha kumpa Rais Samia zaidi ya kumshukuru kwa hatua hiyo ambayo imeafuta kabisa machozi ya watazania wengi hususani wanyonge wenye vipato vya chini.
”Mwaka huu unaelekea ukingoni, tunazidi na tutazidi kuendelea kumpongeza Rais Samia kwa hatua nyingi anazozichukua kuwapunguzia mzigo Watanzania , amefuta vilio vya masikini wengi waliokuwa wakihaha kutafuta hela kuwalipia watoto wao ada,” alisema.
Naje Joyce Damian alisema baada ya hatua ya aliyekuwa Rais mstaafu wa awamu ya Tano marehemu Dk John Magufuli kufuta ada kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, Rais Samia ‘ ameupiga mwingi’ kwa kufuta ada kwa kidato cha tano na sita
Alisema hatua hiyo ameonyesha kulijali Taifa analoliongoza, kwani amewatua mzigo mzito wananchi wake hali iliyopelekea elimu nchini kuwa bure kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita.
“Watanzania watake nini zaidi ya Rais Samia. Niwatake wanawake wenzangu waliopo kila kona ya Tanzania kujitokeza na kuzitangaza kazi nzuri alizozifanya Rais Samia mwaka huu,” alisisitiza.
Aliwataka wanamme wote nchini kulichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa, kwani kitendo alichokifanya Rais kuondoa ada hiyo kinawapunguzia mzigo wa kusomesha watoto waliokuwa nao.
Alisisitiza Kwa kusema watanzania wote wamelipokea suala hilo kwa mikono miwili na zaidi ana anaamini kuwa wakati wote wataendelea kumuunga mkono huku akiwataka kumuombea Dua njema kwa Mungu apate kuwa na afya njema wakati wote ili azidi kuwatumikia.
Mwishooooooooooooooooooo
anchor
Watetezi haki za binadamu
watakiwa kuunganisha sauti
Na Jackline Martin
WATETEZI wa Haki za binadamu wametakiwa kuungana kwa na sauti ya pamoja kutetea haki za binadamu hasa kwa kukemea uvunjifu wa haki hizo ili kila mwenye haki aweze kupata haki yake stahiki.
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam na Mshauri wa Mambo ya Kisheria KKKT- Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Manford Kijalo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kampeni ya masuala ya haki za binadamu na hasa kwa Tanzania katika suala zima la kumiliki na kutumia ardhi iliyoanzishwa na Jumuiya ya kimataifa (UEM).
“Kwetu hapa Tanzania utetezi wa haki za binadamu utajielekeza kwa waathirika wa matatizo ya viwanja /ardhi kwani migogoro imekuwa ni mingi sana,” alisema.
“Haki za binadamu zinatambuliwa ulimwenguni kote, ni misingi ya maadili inayotakiwa kutumika kwa manufaa ya binadamu wote duniani na kwa usawa,” aliongeza Mchungaji Kijalo
Mchungaji Kijalo alisema kwa Tanzania kumekuwa na matatizo mengi na migogoro mingi katika suala zima la umiliki na matumizi ya viwanja/ardhi hasa pale ambapo wahanga alipopoteza ardhi zao kwa njia ya hila kutoka kwa baadhi ya watendaji wakishirikiana na watu wenye fedha.
“Jamii yetu ya kitanzania inategemea sana ardhi kwa ajili ya kuendesha maisha yao, mfano kilimo, ujenzi wa nyumba na uwekezaji mwingine wowote hivyo sisi na UEM tuna wajibu wa kusimama na hawa wahanga ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuinuka na kubaki katika furaha na amani ya matumizi ya ardhi katika nchi yao, ” alisema.
Kijalo aliongeza kuwa kilichoisukuma jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kunakuwa na mifumo thabiti ya ulinzi wa haki za binadamu ni mateso na uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu uliofanyika wakati wa vita ya pili vya Dunia.
Pia Mchungaji Kijalo alisema wataendelea kutoa elimu kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni kuhusu sheria za kupata na kumiliki viwanja, wajibu wa serikali katika masuala ya ardhi na wajibu wa kanisa katika kutatua migogoro ya ardhi na hasa baina ya washarika katika kanisa.
Kijalo aliushukuru uongozi wa UEM kwa utayari wa utume wa kutunza hadhi na utu wa mwanadamu.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapato