March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Korea kusini yaendesha mafunzo kwa wataalamu wa TEHAMA

Na Bakari Lulela,Timesmajira

TUME ya Tehama nchini pamoja na Taasisi inayoshughulika na mambo ya usalama wa mitandao ya Korea kusini yaani Korea Internet and Security Agency(KISA) wamezindua mafunzo ya changamoto na mafanikio ya mambo ya usalama wa mtandao(Cyber security)kwa wataalamu wa taasisi mbalimbali na sekta binafsi ambayo yanafanyika kwa siku tano kuanzia Agosti 11i hadi agosti 15,2025 jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye hoteli ya New Afrika  jijini Dar es salam Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Tehama Dkt.Nkundwe Moses Mwasaga amebainisha kuwa mafunzo hayo yana tafsiri kubwa katika kujenga uchumi wa kidigitali ambao utawavutia wawekezaji na kuleta fursa mbalimbali kwa wananchi wa kawaida.

Dkt.Nkundwe amesisitiza  ili mtu aweze kuwa na  Imani(trust) ya kutumia mifumo hiyo ya akiliunde ni lazima kuwe na mifumo ya usalama wa taarifa binafsi,Ili kulinda faragha za watu na kumlinda mlaji wa mifumo ya kidigitali .

“Kuna jambo jipya limejitokeza sasa hivi na limeanza kuonekana kuwa lina umuhimu mkubwa sasa hivi kupitia mitandao watu  wanaweza wakaingilia mifumo lakini pia wanaweza kumbadilisha mtu fikra zake na kufikiria jinsi wanavyotaka wao huo unaitwa Udukuzi wa fikra na baadhi ya nchi wamesema ni hatari kwa jamii kwa hiyo tumeona ni vizuri wataalamu wetu wakajifunza ujanja gani unatumika na namna gani unavyofanywa”,amesema Dkt.Nkundwe

Aidha Dkt.Nkundwe ametoa shukrani kwa Korea Internet and Security Agency(KISA) kwa kukubali kuendesha mafunzo hayo nchini Tanzania ambayo imepata fursa ya kuhudhuriwa na wataalamu kutoka taasis 33 ambapo watapata ujuzi na kuwasaidia watu wengine.

 ‘Mbinu za watu wabaya mitandaoni zinabadilika kila siku hivyo kupata elimu kutoka kwa nchi nyingine itasaidia kujifunza mambo mapya na Wakorea ni wataalam na watafanya mifumo yetu iwe vizuri zaidi kwa hiyo ni njia ambayo serikali imenuia kujenga uchumi madhubuti wa kidigitali”.amesema Nkundwe

Katika hatua nyingine mtafiti wa Korea Internet and Security Agency(KISA),Minyoung Kim amesema kuna umuhimu wa kutengeneza ushirikiano wa pamoja ili kuzishinda changamoto za mifumo ya kimitandao.

Minyoung ameongeza kuwa “katika nchi yetu Korea Kusini  tumedhamiria kuwa na wataalamu 10,000 wenye uwezo wa kulinda mambo ya mitandao ya kidigitali”.

Nae  mtaalamu wa mawasiliano ya teknolojia ya habari katika kitengo cha ulinzi wa tehama  pia .Venance Mwachabike amefurahishwa na Mafunzo hayo ambayo yatamsaidia katika kuboresha kitengo anachofanyia kazi