Na Joyce Kasiki,Timesmajira Online,Kongwa
AFISA Elimu Wa Mkoa wa Dodoma Gift Kyando ameutaka uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa kufuatilia suala la uandikishaji wa darasa la awali na darasa la kwanza ikibidi kwa kutoza faini ili waweze kufikia lengo la uandikishaji wa madarasa hayo.
Kyando ameyasema hayo wilayani Kongwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyefanya ziara wilayani humo kukagua shughuli za maendeleo ikiwemo suala la elimu kwa ujumla.
Amesema wilaya hiyo inaonekana ipo nyuma katika uandikishaji wa madarasa hayo huku akisema wanapaswa kukimbia zaidi ikiwemo kutoza faini kwa wazazi wanaokaidi kufanya hivyo na hivyo kuchangia uandikishaji huo.
Kwa mujibu wa Afisa Elimu huyo ,hadi kufikia Disemba 31 mwaka jana uandikishaji wa awali darasa la awali ka wilaya ya Chamwino ulikuwa ni asilimia 73.59 ,Bahi 77.38,Chemba 78.38,Jiji 83.70,Kondoa TC 72.83,Kongwa 67.22 na Mpwapwa 74.53 na Kondoa DC 73.04 na hivyo kufanya mkoa kufikia asilimia 75.29.
“Kwa ufupi Kongwa mnakimbia nyuma ya halmashauri zote,mnapaswa kukimbia zaidi ili mzipite halmashauri zote na mfike asilimia 100 ya uandikishaji wa darasa la awali na ikumbukwe kuwa uandikishaji wa darasa la awali ni kigezo cha halmashauri kupata fedha kupitia mradi wa Boost ambao na Kongwa imo katika utekelezaji wa mradi huo.”amesema Kyando
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Omary Nkullo amesema,lengo la Kongwa ni kuandikisha wanafunzi wa darasa la awali 12,909 ,wavulana 6,413 na wasichana6,496 lakini hadi kufikia Disemba 31 mwaka jana walikuwa wameandikisha wanafunzi 4,228 na wasichana 4,445 na kufaya idadi ya walioandikishwa kufikia 8,673 sawa na asilimia 67 ya lengo .
“Asilimia 33 bado hawajaandikishwa ambao kati yao 2,183 na wasichana 2,051 jumla watoto 4,236 bado hawajaandikishwa darasa la awali.”amesema Dkt.Nkullo
Kuhusu darasa la kwanza amesema walilenga kuandikisha watoto 15,694 ambapo wavulana 7,860 na wasichana 7,834 lakini hadi kufikia Disemba 31 mwaka jana watoto 11,091 walikuwa wameshaandikishwa ambapo wavulana 5,468 ambapo 2,392 bado hawajaandiskishwa na wasichana 2,211 na kufanya jumla ya wanafunzi wa darasa la kwanza ambao bado hawajaandikishwa kufikia 4,603.
Kwa mujibu wa Mtaala na Muhtasari wa Elimu ya Awali Toleo la kwanza la 2016,Walengwa wa elimu awali ni watoto wote wenye umri wa miaka mitano wakiwemo wenye mahitaji maalumu.
Hata hivyo amesema,wamepanga kupita nyumba kwa nyumba kwa kutumia mgambo na vijana wa skauti ili kuwasaka ambao bado hawajaandikishwa .
Vile vile amesema kwa elimu maalum walioandikishwa kwa darasa la kwanza ni wanafunzi wanane wavulana watano na wasichana watatu na darasa la awali wameandikishwa watoto watano ambapo kati yao wavulana wanne na msichana mmoja .
Pia amesema watoto waliovuka umri nao wameandikishwa ambapo idadi yao ni 51 kati yao 23 wavulana na 28 ni wasichana .
Sidha,kwa mujibu wa muongozo wa Programu Jumuishi ya Kitaifa ya miaka mitano (PJT-MMMAM) 2021/22-2025/26,kuanzishwa kwa Programu hiyo kumelenga mtoto kulelewa katika afua stahiki zitakazomwezesha kukua katika utimilifu wake na kuwa mwenye tija kwa Taifa.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja