Na Mwandishi wetu Timesmajira online
MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema ujenzi wa Kongani ya Viwanda ya Sino _Tan kibaha (Industrial Park) katika eneo la Kwala Mkoani Pwani unaendelea na utakapokamilika unatarajia kutoa zaidi ya ajira laki moja za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja laki tano.
Msigwa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ameyamebainisha hayo wakati akizungumzia na waandishi wa habari mapema leo Machi 16,2025 masuala mbalimbali ikiwemo Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita katika bandari kavu ya Kwala Mkoani Pwani .
Msigwa amesema pia litakuwa na Viwanda vikubwa 200 na Viwanda vidogo 300 ambapo vitajumuisha sekta mbalimbali ikiwemo usindikaji wa chakula , kemikali ,nguo na dawa.
“Eneo hili ni moja wapo ya miradi ya kimkakati ambao upo Mkoa wa Pwani ukubwa wake ni ekari 250 na linamtaji wa dola za kimarekani millioni 372 sawa na shilingi Billioni 882 “amesema MsigwaAidha amesema kwa sasa mradi huo upo katika awamu ya kwanza huku ujumla ya awamu zote zikitarajiwa kuwa tano.
“Ujenzi wa awamu ya kwanza ulianza Mei 2022 na upo katika hatua za mwisho mpaka sasa kuna Viwanda vitatu ambavyo tayari vinazalisha huku vitatu vikiwa katika hatua za kufunga mitambo”amesema
Ameongeza kuwa eneo hilo linauwezo wa kuzalisha bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani Billioni sita sawa na Trillioni 16 kwa mwaka .
“Serikali itakuwa ikikusanya kwenye kongani hii moja kiasi cha Kodi zaidi ya trillioni 1.2″amesema Msigwa
More Stories
MSIGWA:Mfumo wa usajili waandishi wa habari kidijitali upo mbioni kukamilika
Waandishi wa habari kutambulika kidijitali
Mahundi awataka wanachuo kutoendekeza anasa