Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM
KAMPUNI ya MICO International Halal Bureau Limited, imeandaa kongamano la biashara na wadau wa Hahal litakalofanyika siku ya Jumatano jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Mohamed Matano, alisema MICO ni kampuni pekee Tanzania ambayo inatoa ithibati ya Halal kwa wafanyabiashara na kampuni zinazotoa huduma ndani ya nchi.
Alisema kampuni ya MICO ndiyo inatoa ithibati kwa kampuni na wafanyabiashara wanaozalisha na kutoa huduma hapa nchini.
“Tarehe 14 mwezi wa nane kutakuwa na kongamano la pili la kimataifa katika ukumbi wa kimataifaa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na tunatanarajia kukutana na wadau wa Halal hapa nchini,” alisema.
“Tanzania tunanafasi kubwa ya kupata mapato kupitia Halal Industries katika utalii, katika dawa, famasia na fedha kwa hiyo tutakapokutana na wadau tutajadiliana namna ya kuboresha shughuli za Halal hapa nchini,” alisema
Alisema wadau mbalimbali na viongozi wa serikali watahudhuria kongamano hilo la wadau wa Halali ambalo linakadiriwa kushirikisha washiriki 500 wanaofanya kazi kwenye kampuni mbalimbali.
“Kutakuwa na muda wa B2B yaani mtu mmoja mmoja kukaa na kuzungumza masuala mbalimbali ya Halal kwa hiyo tunaomba wananchi wote wanaopenda kushiriki kongamano hili wajisajili,” alisema
Alisema MICO International Halal ndiyo inasimamia machinjio yote Tanzania kwa kuwafundisha wachinjaji mafunzo ya Halal na kuhakikisha machinjio hayo yanaendeshwa katika misingi ya Halal.
Alisema kampuni hiyo ilipewa idhini ya kuendesha shughuli hiyo na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
More Stories
Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa nchi zinazozalisha kahawa Afrika
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji wakigombania shamba
Ng’ombe 10 wamekufa kwa kupigwa na radi