December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KKT inafanya kazi kwa karibu na BAKWATA

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Injinia Robert Kitundu, amesema kwamba kanisa lao linafanya kazi kwa karibu na Baraza la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) licha ya kwamba wao kazi yao kubwa ni kueneza Injili duniani kote

.Naye Katibu Mkuu Baraza la Kiislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikhe Jabir Nuhu Mruma amesema,

“Sisi Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (Bakwata), tunashirikiana kwa karibu kabisa na madhehebu ya dini mbalimbali likiwamo hili la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Nichukue nafasi hii kufikisha salamu za Mufti wa Tanzania Sheikhe Abubakar Zuber Bin Ally.

Mufti anawatakia kheri KKKT katika maadhimisho yao ya miaka 60 tangu kuzaliwa kwake.

“Sisi kwa pamoja tunawaombea mema viongozi wote wa serikali na kuitakia mema nchi yetu. Sisi viongozi wa dini tutaendelea kuwa mstari wa mbele kuishauri serikali na kushirikiana na serikali ili ifanye kazi nzuri ya kuwatumikia Watanzania,”Amesema Sheikhe Jabir.