Na Irene Fundi, TimesMajira Online
ALIYEKUWA kocha wa makipa wa Klabu ya Simba Muharami Sultan (40) na wenzake 6 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Mashitaka hayo yamesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Merry Mrio na Wakili wa utetezi Daudi Mzeri.
Wengine ni pamoja na Mmiliki wa Kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi seif, Said Matwiko mkazi Magole, Maulid Mzungu maarufu mbonde (54) mkazi wa kisemvule na John John maarufu Chipanda (40) ambaye jukumu lake kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sport Academy na Sara Joseph.
Mwanga ameieleza mahakama kuwa watuhumiwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya usafilishaji wa madawa ya kulevya
Katika hati ya mashitaka imeeleza kuwa mnamo tarehe 27,2022Â Ilala Dar es Salaam walikutwa wakisafirisha madawa ya kulevya aina heroin yenye uzito wa kiliglamu 27.1.
Pia shitaka la pili wanatuhumiwa kulitenda mnamo tarehe 4,11 2022 ndani ya Wilaya ya Mkuranga Pwani walikutwa wakisafirisha madawa aina heroin yenye uzito wa kiliglamu 7.79.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo Hakimu Mrio amewaeleza watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikilizwa kesi hiyo.
Wakili Mwanga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaemdelea.
Kesi hiyo imehairishwa hadi Desemba 5,2022 kwa ajili ya kutajwa na watuhumiwa wamerudishwa rumande.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba