November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kiwanda cha Marmo chatoa wito wajenzi kununua bidhaa zake

Meneja Utawala wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd Bw. Binthony Kulliga akitoa taarifa ya kiwanda hicho kilichopo Iyunga Mbeya kwa Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa zaiara ya kimafunzo kulia ni  Salim Jessa  Mkurugenzi wa kiwanda hicho.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd akitoa maelezo kwa Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa zaiara ya kimafunzo.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd akionesha moja ya meza zilizotengenezwa kwa mawe ya asili  kwa Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa zaiara ya kimafunzo.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd akionesha moja ya bidhaa zilizotengenezwa kwa mawe ya asili kwa ajili ya mapambo ya makaburi   kwa  waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa zaiara ya kimafunzo.

Baadhi ya waandishi wa kitembelea kiwanda hicho

Baadhi ya mawe ya asili yanayotengeneza bidhaa  mbalimbali kiwandano hapo. 

Baadhi ya mashine zinazotumika kutaka mawe kwa ajili ya kutngeneza bidhaa hizo.

…………………………

UONGOZI wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd kilichopo jijini Mbeya umetoa  wito  kwa taasisi mbalimbali za Serikali, binafsi na wadau mbalimbali zinazojihusisha na ujenzi wa majengo kuunga mkono kwa kununua bidhaa  bora za ujenzi zinazozalishwa kiwandani hapo ili kujenga uchumi ulio imara kwa viwanda vya ndani na kuleta tija katika kukuza uchumi wa taifa.Kauli hiyo imetolewa na Meneja Utawala wa Kiwanda hicho Bw. Binthony Kulliga wakati akizungumza na waandishi wa habari walioongozana na maofisa  wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni ziara ya mafunzo kufuatia semina ya siku 5 iliyoandaliwa na kuratibiwa na BoT mkoani Mbeya.Amesema mradi huu siyo tu unautangaza mkoa wa Mbeya katika ramani ya Dunia bali pia Taifa  kwa kuzingatia kuwa bidhaa hii ni bora na inaendelea kuenea katika soko la ndani na la  Kimataifa  hivyo kutoa fursa ya kuongeza uzalishaji ili kukidhi soko la ndani ya nje ya nchi.Kulliga ametoa mfano kwa taasisi kama TBA, NHC, NSSF na nyingine ambazo zinashiriki katika ujenzi wa majengo kuwa ziaweza kuunga mkono juhudi za kiwanda hicho kwa kununua bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo  hasa kipindi hiki ambacho Serikali imehamia mkoani Dodoma na inaendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali.”Mradi huo ni wa kipekee nchini Tanzania kutokana na teknolojia yake ambapo vyuo vya hapa nchini havina mitaala katika silabi zao juu ya uzalishaji wake,” Amesema Bw Kulliga.Aidha Bw. Binthony Kulliga ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake thabiti kwa kuwa  umewezesha kiwanda hicho cha kukata, kung’arisha na kuuza bidhaa zinazotokana na mawe ya asili aina ya Marbe na Granite yanayopatikana hapa nchini kupiga hatua kubwa.Amefafanua kuwa  mradi huu ni wa kizalendo kwa maana ya Watanzania, hivyo mipango, mikakati na jitihada za kizalendo za kuinua uchumi zinazotokana na uongozi thabiti wa Rais Samia ambao umetuwezesha kupiga hatua.”Mradi huu ulipokuwa ukianza ulikuwa na wafanyakazu wazalendo wapatao 35, baada ya ujenzi wa kiwanda tayari mradi umekuwa na wafanyakazi wazalendo wasiopungua 100 kwa sehemu ya kiwanda na migodini,” Amesema Kulliga.Amesema, kwa ujumla asilimia 80 ya walioajiriwa ni wazalendo na wanatarajia kadri uzalishaji utakavyoongezeka machimboni na viwandani kampuni itaongeza ajira zaidi.Kulliga pia  ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa mikakati yake ya kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari za biashara, uchumi na fedha kwani hatua hiyo itajenga waandishi wa habari  kuwa wabobezi wa habari za uchumi na biashara na fedha.Mafunzo hayo ya siku tano ambayo yalianza Februari 14,2022 na yanatarajiwa kufungwa Februari 18,2022 yanawajumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yakiratibiwa na kuendeshwa na BoT.