December 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kituo chochote cha mafuta kinaweza kufunga mifumo ya gesi asilia

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA ) imesema  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limefanya marekebisho ya viwango vya ubora ambapo kituo chochote Tanzania kinaweza kuweka mradi wa ufungaji wa mifumo ya gesi asilia (CNG).

Akizungumza na waandishi habari kwwnye banda la EWURA katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam,Meneja uhusiano na Mawasiliano wa EWURA Titus Kaguo amesema hatua hiyo ni kurahisisha uwekezaji wa vituo vya gesi asilia kama nishati mbadala wa matumizi ya mafuta kwwnye magari.

Kwa mujibu wa Kaguo ili CNG iweze kutumika nchi nzima lazima iende kwa vituo mkoa hadi mkoa  tofauti na bidhaa nyingine inavyoweza kuwekezwa mahali popote.

“Hili ni wazo la nishati mbadala wa matumizi ya mafuta kwenye magari na hii ni kutokana na hali ya upatikanaji wa mafuta duniani kote .” Amesema Kaguo

Ameongeza kuwa”Kwa hiyo tunaendelea kuhamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye vituo vya gesi asilia lakini pia tunahamasisha wananchi kuanza kubadilisha mifumo yao kwenda kwenye gesi asilia ili tuhame sasa kutoka kwenye mafuta.”

Aidha Kaguo amesema pia wanayatumia maomeaho hayo kuwaeleza wananchi kutoka kwenye nishati chafu ya kupikia na kwenda kwenye nishati safi ya kupikia ili kuokoa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Elimu hii imeanza kuzaa matunda maana kuna baadhi ya akina mama wanakuja kuulizia utaratibu wa kuunganishiwa gesi kwenye nyumba zao nasi tunawapa maelekezo mahali pa kwenda kuhudumiwa.” Amesiaitiza

Pia amesema wapo wanaofika kwenye banda hilo kujua jinsi ya kupata leseni ndogo za wakandarasi wadogo .

“Wizara iliipa EWURA mamlaka kutoa leseni ndogo za wakandarasi ambazo zina madaraja mbalimbali ,na hao ndio wengi hufika kwenye banda letu kuuliza wanapataje hizo leseni,nasi tunawaelekeza jinsi ya kuzipata kwenye mtandao .”amesema