January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kituo cha umeme Nyakanazi chaimarisha upatikanaji umeme Wilaya nne

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Serikali imesema kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi mkoani Kagera imepelekea kutenganisha matumizi ya umeme katika wilaya za Bukombe, Mbogwe, Biharamulo na Chato jambo ambalo limesaidia kila wilaya kujitegemea na pia kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme katika Wilaya ya Biharamulo.

Naibu waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa katika Wizara ya Nishati na Waheshimiwa Wabunge akiwemo Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Eng. Ezra Chiwelesa.

Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa TANESCO inaendelea na matengenezo ya kuimarisha miundombinu ya kusafirishia na kusambazia umeme katika Wilaya ya Biharamulo ili kuwe na umeme wa uhakika