January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kim Kardashian, Kanye West mbioni kuachana

CALIFORNIA, Marekani

NYOTA wa vipindi vya Television na msanii nchini Marekani Kim Kardashian inaripotiwa yupo mbioni kuachana na mume wake Kanye West, kwa kile kinachodaiwa hali si shwari ndani ya nyumba.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya burudani nchini Marekani, ukiwemo mtandao wa Page Six umeripoti kuwa huenda Kim Kardashian akadai talaka yake kutoka kwa Kanye West, baada ya kudaiwa kutoridhika na mienendo ya Mume wake ikiwemo kuutangazia umma kuhusu mambo ya ndani ya familia.

Kim mwenye umri wa miaka 39 raia wa Marekni amedai kitendo cha mumuwe kutangaza ishu kutaka kutoa mimba mbele ya umma kimemuumiza sana, hivyo anachosubiri Kanye aweze kukaa sawa ili afanye maamuzi hayo.

Hata hivyo Kim amedai kumekuwa na misuko suko yeye na mumewe kutokana na kumueleza kipindi cha The Kardashians kitamalizika mwakani.