Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki amesema mradi wa uboreshaji wa barabara za vijijini kwa ushirikishaji na ufunguaji wa fursa za kijamii na kiuchumi (RISE) unaotekelezwa chini ya TARURA utajenga barabara Km 535 katika mikoa 4 nchini.
Kairuki ameyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa barabara za Mtili – Ifwagi (Km 14) na Wenda – Mgama (Km 19) mkoani Iringa kwa kiwango cha Lami iliyofanyika kwenye Manispaa ya Iringa tarehe 20.06.2023
Amesema mradi huu umeanza Nov 2021 na utakamilika June, 2027 utahusisha ujenzi wa barabara za Mikoa Km 135 zilizoko chini ya TANROAD, ujenzi wa barabara za Wilaya Km 400 za TARURA, Matengenezo ya Maeneo korofi km 4,500 -TARURA, Matengenezo ya kawaida ya Barabara kwa kutumia vikundi km 23,000- TARURA pia kupitia mradi huu ajira 35,000 zinatarajiwa kupatikana.
Kairuki amebainishea uboreshaaji wa barabara za vijijini kupitia mradi huu ni dhahiri kuwa utachangia katika kupunguza umaskini kwenye maeneo yatakayopitiwa na mradi, utawezesha ufikaji kwenye maeneo ya uzalishaji (Mashambani, maghala na masoko ya mazao) na pia utakuza kilimo na kufugua fursa mbalimbali za kiuchumi ambapo jamii husika itashirikishwa.
Mradi unatarajiwa pia kushirikisha jamii katika kazi za Ujenzi wa Barabara hususani matengenezo ya kawaida (routine maintenance) kwa kutumia vikundi vinavyoundwa na watu wanaoishi katika maeneo ya Jirani na barabara pamoja na kuandaa mfumo wa kutumia takwimu kwa ajili kutoa vipaumbele kwenye ujenzi wa barabara za vijijni nchini amesisitiza.
Aidha Kairuki amewaagiza Watendaji wa TARURA kuhakikishs wanasimamia kwa karibu Wakandarasi na ili mradi ukamilike kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa na fidia kwa waathirika wa miradi inayofuata zifanyika mapema kama ilivyofanyika kwa mradi huu, ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi.
Pia amesisitiza utaratibu wa kutumia vikundi katika matengenezo ya barabara unakuwa endelevu. Utaratibu huu uzingatie makundi mbalimbali (Vijana, wazee na watu wenye ulemamvu.
More Stories
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali