Na Allan Vicent, TimesMajira Online Sikonge
WAKAZI wa Kata za Igigwa na Usunga katika Halmashauri ya Wilaya Sikonge Mkoani Tabora wamemshukuru Rais Dkt Salmia Suluhu Hassan kwa kurahisisha upatikanaji pembejeo na kwa bei nafuu hali iliyopelekea wakulima wengi kuinuka kiuchumi.
Hayo yamebainishwa jana na Viongozi na Wanachama wa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku katika kata hizo walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari waliowatembelea ili kujionea maendeleo ya shughuli za kilimo vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi Imala-Upina (Amcos) kilichopo katika Kijiji cha Tumbili, Kata ya Igigwa wilayani humo, Mrisho Ali amesema kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani wakulima wengi wamehamasika sana kulima tumbaku.
Ametaja sababu kubwa kuwa ni kurahisishwa upatikanaji pembejeo kwa wakulima na kuwawezesha kupata mbolea ya ruzuku kwa bei nafuu tofauti na hali ilivyokuwa huko nyuma, hili limefanya kilimo kuwa na tija kubwa kwa mkulima.
‘Msimu wa kilimo uliopita 2022/2023 tulijiwekea lengo la kuzalisha kilo laki 9 za tumbaku kupitia wanachama wetu 353 lakini kutokana na kupata pembejeo kwa wakati na kwa bei nzuri tulivuka lengo kwa kuzalisha kilo mil 1.15’, amesema.
Katibu Meneja wa Amcos hiyo Juma Mlega ameeleza kuwa malengo yao kwa mwaka huu ni kuzalisha zaidi ya kilo mil 1.2 ambapo matarajio yao ni kupata zaidi ya sh bil 2.8 huku akibainisha kuwa malengo hayo yameendelea kupanda kila msimu.
Amesisitiza kuwa kilo mil 1.15 zilizozalishwa msimu uliopita na kukiingizia chama chao zaidi ya sh bil 2.5 zimewezesha wakulima kujenga nyumba mpya za kisasa, kununua magari, kusomesha watoto wao sekondari na wengine hadi chuo kikuu.
Ameongeza sababu ya mafanikio hayo kuwa ni kuboreshwa sekta ya kilimo, kufuata kanuni za kilimo bora, hali ya hewa rafiki (mvua za wastani), upatikanaji pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu, upatikanaji wa masoko na kuvuna tumbaku ubora.
Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi Usunga (Amcos) Ramadhan Mbesi amefafanua kuwa maboresho makubwa ya sekta ya kilimo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya 6 yamewezesha wakulima wa tumbaku katika wilaya hiyo kunufaika zaidi.
Amebainisha kuwa kwa mwaka jana walikisia kuzalisha kilo laki 6.5 lakini wakavuka lengo kwa kuzalisha kilo mil 1.16 na mwaka huu wamejiwekea lengo la kuzalisha kilo mil 2 ambazo wakiziuza watapata zaidi ya sh bil 4.
Naye Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Tabora (WETCU) Samwel Jokeya ameshukuru serikali kwa kurahisisha upatikanaji pembejeo kwa vyama vya wakulima na kuanzisha utaratibu wa kusambazwa mbolea ya ruzuku kwa wakulima vyama vya wakulima.
Ameongeza kuwa serikali imemsaidia mkulima sana kwa kumtafutia masoko ya uhakika cha zao la tumbaku na kumrahisishia suala zima la upatikanaji pembejeo tofauti na zamani.
Ametaja changamoto pekee inayowakabili kwa sasa kuwa ni ukosefu wa pembejeo za uhakika na ukosefu wa kamba ya kufungia mabelo ya tumbaku inayovunwa kwa ajili kusambazwa hivyo akatoa wito kwa wakulima kuwa watulivu wakati hilo likiendelea kushughuliwa.
More Stories
5 “best” Bitcoin Online slots games
Best Web based casinos Norway Your own #1 Norwegian Online casinos 2024
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere