December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kilili awataka wanawake kujikwamua kiuchumi

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MJUMBE wa Baraza la Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Elizabeth Kilili (Mama Zoa zoa )amewataka Wanawake Kipawa kujikwamua kiuchumi kwa ajili ya kubuni biashara zitakazowaingizia mapato.

Kilili, ameyasema hayo katika kata ya Kipawa Tawi la Kidarajani wakati wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya wanawake UWT ulioandaliwa na Tawi hilo.

“Nawaomba wanawake wenzangu wa Kipawa mjikwamue kiuchumi mzalishe bidhaa bora mkuze mitaji yenu muweze kukuza soko ,marufuku pesa za mikopo kuzitumia katika shughuli za sherehe badala yake mkikopa mtumie katika ujasiriamali “alisema Elizabeth.

Dkt. Elizabeth amewataka Wanawake mkopo wasinunulie kitu chochote badala yake watumie katika biashara zao walizobuni ili waweze kujiongezea kipato kitakachowakwamua kiuchumi.

Aidha amewataka wanawake wasichukue mkopo bila elimu ya ujasiriamali ambapo alisema ukichukua mkopo bila elimu uwezi kufanya malengo uliokusudia badala yake unaweza tumia katika shughuli tofauti na malengo yaliokusudiwa.

“OFISI yangu ipo tayari kutoa elimu bure kwa wanawake inayohusiana na ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi tuweze kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wanawake tujishughulishe amna kurudi nyuma”amesema .

Amewataka wanawake wa Wilaya ya Ilala kuwa na upendo na kushirikiana pamoja katika uzalishaji Mali ili malengo yao yaweze kutimia.

Akizungumza na wanawake wa UWT Kidarajani amewachangia jezi kwa ajili ya mazoezi ya JOGING seti moja wanawake wa UWT ili waendelee kuamasisha Jumuiya ya wanawake ili waongeze Wanachama katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.