January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kikao kazi kuhusu bomba la mafuta la TAZAMA kufanyika

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wizara ya Nishati inatarajia kufanya kikao kazi Cha Mawaziri kutoka Tanzania na Zambia kitakachojadili ushirikiano baina ya nchimbi hizo mbili katika ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la TAZAMA na Sekta ya Nishati Kwa ujumla wake.

Kikao hicho kitatathimini utekelezaji wa masuala ya ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la TAZAMA kama ilivyokubalika katika kikao Cha kwanza Cha Wizara hizo tatu kilichofanyika mwezi Desemba, 2022 jijini Dar es Salaam baada ya serikali ya Zambia kuamua kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta safi badala ya mafuta ghafi.

Hayo yamesemwa Waziri wa Nishati January Makamba wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema uwepo wa kikao hicho ni Moja ya mashirikiano mazuri kati ya nchi hizo mbili na pia ni muendelezo mahusiano mema unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema.

“Tutapokea taarifa Mapendekezo ya ujenzi wa bomba jipya la TAZAMA, bomba hili lilijengwa mda mrefu na lina kipenyo chembamba , kwasababu biashara imekua na mahitaji ya mafuta yameongezeka imeonekana kwamba kuna haja ya kujenga bomba Pana zaidi litakaloweza kusafirisha pia bidhaa nyingine zaidi ya dizeli”

“Bomba la TAZAMA lina urefu wa Km 1.710 kutoka Kigamboni-Dar es Salaam hadi Indeni -Ndola Zambia, changamoto kubwa ni ulinzi na usalama wa Bomba hilo baada ya kuanza kusafirisha mafuta yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi”

Makamba amesema Ufanisi wa bomba hilo la TAZAMA utasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta lakini pia kuweza kuisaidia mikoa ya kusini mwa Tanzania kupata mafuta kwa unafuu kwasababu kwenye mpango mpya kutakua na matoleo ya kushusha mafuta kwenye mikoa ya morogoro, iringa, mbeya na Songwe hivyo barabarani kutakua na magari machache zaidi na gharama za usafirishaji mafuta zitakua chini zaidi ambapo wananchi wa mikoa hiyo watapata mafuta kwa urahisi zaidi.

Pia Makamba amesema katika kikao kazi hicho, kutajadiliwa namna ya upanuzi wa bomba hilo la TAZAMA kwaajili ya kupitisha aina zote za mafuta safi na sinsi ambavyo mikoa ya kusini mwa nchi inaweza kupata mafuta ya kupikia kupitia bomba hilo na pia bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Tanzania kwenda Zambia.

“Bomba hili sasahivi linasafirisha takribani lita milioni 90 kwa mwezi hivyo kama litakua na ufasini, wenzetu wa Zambia wataendelea kuitegemea Bandari yetu ya Dar es Salaam kuingizia mafuta nchini mwao na tukijenga bomba kubwa zaidi vilevile Bandari ya Dar es Salaam itapata soko kubwa zaidi kwaajili ya mafuta yanayokwenda Zambia na hatimaye kwenda Congo” Amesema Makamba.

Kuhusu Bwawa la Mwalimu Nyerere, Makamba amesema Ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kiachotosheleza kuzalisha umeme kwenye bwaa hilo.

Amesema Kina Cha bwawa lolote lile ni mita 184 kutoka usawa wa Bahari, kina kinachotakiwa kufikiwa ili uanze kuzalisha umeme ni mita 163 kutoka usawa wa Bahari na siku ya Jana imefikia mita 163.61.

Makamba amesema Hadi sasa mradi wa kufua umeme rufiji Julius Nyerere unaendelea kwa Kasi kubwa na sasahivi ambapo umefikia asilimia 89 na Hadi kufikia mwezi Julai mradi huo utafikia asilimia 90.

“Huko nyuma kumekuwa na hofu kubwa ya je maji yatajaa kuweza kuzalisha umeme katika bwawa hilo, tulikadiria tutakuwa na misimu mitatu ambayo ndiyo itatosheleza kujaza bwawa hilo lakini ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kiachotosheleza kuzalisha umeme kwenye bwawa la Julius Nyerere”.

Pia Makamba amesema Kina Cha bwawa lolote la Nyerere ni mita 184 kutoka usawa wa Bahari, kina kinachotakiwa kufikiwa ili uanze kuzalisha umeme ni mita 163 kutoka usawa wa Bahari na Hadi kufikia siku ya Juzi wamefikia mita 163.61.

Aidha Makamba amesema kazi ya ufungaji mitambo inaendelea na mnamo mwezi wa pili wataanza kufanya majaribio ya kuzungusha mitambo kwa maji.

“Imani yetu ni kwamba mwezi wa 6 mwakani tutaanza kutoa umeme pale Julius Nyerere na kuingiza umeme wa kwanza kwenye gridi ya Taifa”

Kuhusu Ujazo wa bwawa la Julius Nyerere Makamba alisema ujazo ni mita za ujazo Bilioni 30 Hadi kufikia Juzi maji yaliyoingia mule ndani ni mita za ujazo Bilioni 13. 8 ambao ni sawa na asilimia 43.