Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. SACP Ismail Mlawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wataalam wa Wilaya hiyo, kilicholenga kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa katika Wilaya hiyo Jijini Mbeya. Kikao kiliratibiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu na kufanyika tarehe 24 Mei, 2022. Mratibu wa Maafa Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Maduhu akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho. Afisa habari Wilaya ya Kyela Bw. Fredy Kabutu akiongoza kikao kazi cha Wataalam wa Wilaya hiyo, kilicholenga kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa katika Wilaya hiyo. Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Mwatima akiwapitisha wajumbe wa kikao kazi hicho (hawapo pichani) wakati wa kuujadili Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya. Sehemu ya wajumbe wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya ya Kyela wakijadiliana wakati wa kazi za makundi. Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi hicho wakiendelea na majadiliano katika makundi. Mwakilishi kutoka Msalaba Mwekundu Kyela, Bw. Zawadi Jackson akiwasilisha kazi ya kundi lake mara baada ya majadiliano wakati wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya hiyo. Mjumbe wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Kyela Bw. David Masanja (Afisa Kilimo) akiwasilisha kazi ya kundi lake mara baada ya majadiliano wakati wa kikao kazi hicho. Mwakilishi kutoka Taasisi ya SONGWECOM Bw. Ghoyela Mpangala akiwasilisha kazi ya kundi lake mara baada ya majadiliano wakati wa kikao kazi hicho. Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. SACP Ismail Mlawa (wa pili kulia waliokaa) pamoja na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya hiyo. Post Views: 324 Continue Reading Previous Serikali, wadau na jamii washauriwa kuweka nguvu upatikanaji wa vifaa vya hedhi kwa watoto wa kikeNext Vyuo vikuu nchini vyatakiwa kutenga fedha kugharamia masuala ya utafiti na ubunifu More Stories Habari Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani January 22, 2025 Judith Ferdnand Habari Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini January 22, 2025 zena chitwanga Habari TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best January 22, 2025 Jackline Mkota
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best