
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Mara
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amewasili katika mkoa wa Mara leo Mei 14, 2026 tayari kwa kuanza ziara yake ya siku tatu katika mkoa huo.
Wakati akiwasili, Kihongosi amepokelewa na wananchi wa Mkoa wa Mara wakiongozwa na maafisa usafirishaji ‘Bodaboda’ ambapo alipokelewa katika eneo la Nyabange wilayani Butiama na kuelekea katika Ofisi za CCM katika mkoa huo.

Aidha akiwa katika ofisi hizo, amepokelewa kwa kuvishwa skafu, kusaini katika kitabu cha wageni pamoja na kukagua ukumbi wa chama CCM uliopo katika ofisi hizo.
Leo ikiwa ni siku yake ya kwanza katika katika ziara mkoani humo, kihongosi atakagua uhai wa chama kwa kutembelea mashina ya CCM katika mkoa huo na kufanya mkutano wa hadhara kwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi, mkutano utakaofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo.


More Stories
Mbeya City Expo yaelimisha wananchi bidhaa bandia
TASAC ,NBS zashirikiana sensa vyombo Majini
Kihongosi:Viongozi msitunishiane misuli