November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kigahe:TRA toeni Elimu kwa wananchi kuhusu misamaha ya Kodi zana za Kilimo

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

NAIBU Waziri wa Viwanda na biashara Exaud Kigahe ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha inatoa Elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu misamaha ya Kodi hasa inayohisiana na masuala ya kilimo.

Kigahe ameyasema hayo mkoani Mbeya katika maonyesho ya kitaifa na kimataifa ya nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Makangale mara baada ya kutembelea kwenye Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

“Nakushukuru Sana kwani moja umesema kwenye eneo la vitenge ilikuwa kero Kwa muda mwingi na hapa lazima tujuwe watanzania wezangu kwamba lengo la Serikali ni kuhamasisha uzalishaji moja nikutaka pamba inayozalishwa hapa nchini ingetuma yote ili kuongeza thamani na ndio maana kumekuwa na punguzo la Kodi lakini mahitaji yanaweza yasijitolesheze.Amesema

“Viwanda vyetu vya ndani lazima tuweke uwiano sawa pamoja na kuvilinda Viwanda vya ndani lakini pia kwasababu tunajua mahitaji yanaweza yasitosheleze na uzalishaji wetu wa ndani kwahiyo lazima turudi na kuweka uwiano kwamba pamoja na kulinda Viwanda vya ndani ambavyo vinazalisha kutumia marighafi tuliyonayo tunayolima Kwa maana sekta ya pamba lakini ili tutosheleze mahitaji ya walaji lazima tuone namna ya wanaoingiza nguo kutoka nje hivyo nashukuru sana.”Amesema Kigahe

Nakuongeza kuwa “tunashukuru sana Wizara ya fedha na TRA tumejadiliana ili kupunguza kidogo ili Kodi waliyokuwa wanatozwa waingizaji bidhaa za vitenge na kanga kutoka nje tunaamini pamoja na maboresho tunayoendelea nayo tunaona lazima tubalasi hivi vitu ili viende pamoja lakini zaidi niendelee kuwashukuru kama nilibyosema mnatoa elimu nzuri lakini tuendelee kutoa elimu zaidi “amesisitiza Naibu Waziri Kigahe

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kodi Kwa mlipa Kodi na huduma elimu TRA Richard Kayombo Amesema wamepunguza baadhi ya Kodi na wanatoa taarifa Kwa wananchi kwamba Kwa miaka iliyopita kulikuwa na changamoto kwenye eneo la uletaji wa vitenge ambavyo vinatumika na watu wengi nchini ambavyo vingine vinazalishwa na pamba ambayo imetokana na kilimo hapa nchini hivyo wale wanaoagiza Kodi imepunguzwa na kiwango cha namna ya kukadilia nayo imepunguzwa ili mtu aweze kupata nafuu anapoingiza bidhaa nakuondoa kabisa magendo.

Pia Amesema kuwa wanayabeba maonyesho hayo Kwa uzito wa hali ya juu na uzito wa kipekee na mkulima anafahamu na kuendelea na shughuli zake za kilimo nakujua faida zake nizipi pindi akiwekeza kwenye sekta mbalimbali na bidhaa za mtaji za kuwekeza Hazina Kodi ya aina yeyote hivyo wananchi wajitokeze kwenye maonyesho hayo na watapata huduma mbalimbali na mtu anayetaka kukadiliwa pia huduma ipo kwenye maonyesho hayo.