December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kigahe akabidhi mitungi ya gesi kwa wanawake

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MBUNGE wa Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe, ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara amekabidhi mitungi 500 ya gesi kwa wanawake wa jimbo hilo yenye thamani ya sh.milioni 50, zilizotolewa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Pia, amesema amejipanga vizuri kumuunga mkono Rais Dk. Samia, katika kutunza mazingira na kuondokana na uharibifu, kwa kuendelea kuwawezesha wananchi na kuwahamasisha kutumia nishati safi kwa wanawake wa jimbo hilo.

Akizungumza jimboni humo jana, wakati wa kongamano hilo, Mbunge Kigahe amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kutoa fedha za kununua mitungi hiyo ya wananchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono kwa kuhamasisha nafasi hiyo.

“Tunamshukuru sana Rais Dk. Samia, kwa upendo wake huu mkubwa, kwani alionao changamoto iliyopo ni mabadiliko ya tabia ya nchi, inayotokana na ukataji kuni, mkaa na maendeleo ya viwanda, hivyo kuwasaidia wananchi kuepukana na Nishati haribifu,” amesema.

Akifungua kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendegu, amempongeza mbunge huyo, kuendelea kutekeleza ajenda ya Rais Dk.Samia, ya kutunza mazingira kwa kuhamasisha nishati safi ya gesi na mkaa mbadala, kuachana matumizi ya kuni.

Amesema athari za mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotokana na uhabifu wa mazingira ya ukataji kuni za kupikia na kutengeneza mkaa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx gas, Benoit Araman amesema wanamuunga mkono Rais Dk.Samia kufikisha nishati safi kwa wananchi.0000