Na Esther Macha,Timesmajira Online,Mbeya
IMEELEZWA kuwa uwepo wa shule binafsi ya mchepuo wa kiingereza ya Kelly’s kijiji cha Nyang’uru Kata ya Mapogoro wilayani Mbarali Mkoani kumechochea jamii ya wakulima na wafugaji kuwekeza katika elimu jambo linalopelekea dhana za kuwatumikisha katika ufugaji kuanza kutoweka.
Mkurugenzi wa Shule hiyo ,Kennedy Lutambi amesema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na msukumo wa kuwekeza elimu Wilayani humo kwa lengo la kusaidia Serikali katika kusaidia jamii hiyo.
”Nimelenga kuwekeza kwenye elimu katika kijiji hicho ni kutokana na kuwepo kwa maono ya kusaidia suala la elimu kwa jamii iliyosahaulika na kuhamasisha umuhimu wa elimu kwa kizazi cha sasa na kijacho huku tukitoa kipaumbele pia kwa watoto wa makundi maalum kama walemavu ”,amesema.
Amesema kuwa uwekezaji katika elimu unahitaji sapoti ya maeneo husika na kwmaba kutokana na mwamko kwa wananchi kwa sasa idadi ya wanafunzi imengezeka kutoka saba mpaka wanafunzi 377 .
”Panapokuwa na mafanikio Changamoto hazikosi kwa sisi wamiliki tumeona mfumo wa utitili wa tozo umekuwa mwiba sana Jambo linatulazimu kupandisha ada ili kuweza kumudu gharama za uendeshaji ”amesema.
Lutambi amesema kutokana na changamoto hiyo wanaiomba Serikali kuangalia mifumo mizuri ya Sera ya elimu ambayo itakuwa wezeshi kwao kwa kupunguza utitili wa tozo kutokana na mchango wao mkubwa katika Sekta ya elimu.
Mwalimu Mwanzilishi wa Shule Ayoub Kibona amesema kuwa kwa sasa wazazi wameelimika kwa kuwekeza kwenye masuala ya elimu kwa vijana
Amesema kuwa katika kuongeza ufanishi na ushirikiano mzuri wameweza kuchangia shughuli mbalimbali za kichamii hususan kuchangia madawati 300 katika Shule msingi Mabadaga Wilayani humo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu