Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameitaka manejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC kuimarisha ushirikiano ili kuboresha ubora wa Huduma kwa wananchi
Dkt. Mollel alitoa wito huo wakati alipokutana na Menejimenti ya Hospitali hiyo na kuwa pongeza kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuhudumia wananchi wa kanda hiyo.
Dkt. Mollel alisema kuwa azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni wananchi kupata Huduma bora na sio bora Huduma.
“Hivyo kufikia ubora wa Huduma katika hospitali hii lazima muwe na ushirikiano wa katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi wanao fata Huduma hapa”, alisisitiza Dkt. Mollel
Aidha aliwapongeza na kuwatia moyo kwa kuendelea kutoa Huduma kwa wananchi wa kanda hiyo ambapo amesema yeye na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wapo kuhakikisha wanatatua changamoto zinazowakabili ili kuhakikisha ubora wa Huduma unapatikana kwa wingi.
Naye Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC, Profesa Gileard Masenga alimshukuru Dkt. Mollel kwa ujio wake na kuwatia nguvu katika kuendelea kutoa Huduma katika hospitali hiyo.
“Nikuahidi tutahakikisha tunasimama ubora wa huduma katika hospitali yetu ili kufikia azma ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa Huduma bora kwa wananchi”, Alieleza Prof. Masenga.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda