December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kayogolo Makamu Mwenyekiti mpya Halmashauri ya Wilaya Nkasi

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Nkasi

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa limemchagua Stephen Kayogolo kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye ataongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akitangaza matokeo hayo leo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu amesema kuwa kwa mujibu sheria Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja.

Amesema kuwa jumla ya kura 34 zimepigwa kati ya hizo kura za ndiyo ni ni 31 zilizoharibika ni 3 na nyingine zote ni za ndiyo .

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti huyo wa Halmashauri hiyo aliyechaguliwa,Diwani wa Kata ya Isale , Stephen Kayogolo amesema kwa nafasi aliyopewa na kuaminiwa ameomba waendelee kumshauri na kumtumia kwa maslahi mapana ya halmashauri na kuwa sehemu nzuri ya kumshauri Mwenyekiti wao Pankras Maliyatabu.

“Nitaendelea kujenga mshikamano na umoja baina yetu Madiwani, ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wote ngazi ya halmashauri, mimi ni binadamu kwa nafasi ambayo mmeniamini naombeni mnitumie katika kunishauri kwa maslahi mapana ya halmashauri yetu,sasa kama kuna jambo la kushauri ni vizuri kuelezana,”amesema Makamu Mwenyekiti Kayogolo.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Willium Mwakalambile
Kwa upande wake amesema kuwa uchaguzi uliofanyika wa kumpata Makamu Mwenyekiti mpya unaenda kuwa chachu kwa Madiwani katika kushirikiana kwa pamoja katika usimamizi wa kazi za halmashauri.

amesema kuwa ushirikiano wa Madiwani wilaya Nkasi ni mkubwa na kuwezesha kupata asilimia 85 ya makusanyo na kuwa sasa ana imani kuwa hiyo asilimia 15 iliyobaki wataikamilisha katika msimu wa mwaka 2023-24 na kuwa uhakika huo upo na watendaji kwa upande wao wamejifua vyema kuyafikia malengo.

Hili ni baraza la robo ya Nne ya mwaka 2022-23 na kukamilisha mwaka kuingia robo ya kwanza ya mwaka mpya.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu akitoa ufafanuzi wa jambo mara baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa makamo mwenyekiti wa jalmashauri
madiwani wakiwa kwenyr baraza la Madiwani wakipitia taarifa mbalimbali za robo ya Nne ya mwaka