Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mwenyekiti wa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mohamed Kawaida amefungua shina la UVCCM liitwalo NMC Kawaida lililopo CCM katika Kata ya 14 Wilayani Temeke lengo ikiwa tawi hilo liweze kutambulika na Chama
Akifungua shina hilo leo wakati wa Ziara yake Wilayani hapo, Kawaida amesema kufunguliwa kwa shina hilo kutaleta chachu kwa uhai wa chama kuhakikisha CCM inazidi kuwa imara.
“Nimefurahi sana kuona shina hili kimepewa jina kwa maana mzee Kawaida ameniongezea nguvu, najua vijana mna changamoto nyingi hivyo sisi kama viongozi wa taifa hatuna budi kuzitatua changamoto hizo.”
“Bahati nzuri nimeambatana na viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa wilaya hii ndugu Martinyi, changamoto kwa vijana hasa wa shina hili amezisikia hivyo hana budi kuelezea na kuzitatua,” amesema Kawaida.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, ndugu Martinyi amesema amezisikia changamoto za shina la Kawaida CCM kata 14 Temeke, atazifanyia kazi kwani fedha zipo kwa makundi ya vijana, wanawake na wenye uhitaji maalumu,” amesema Martinyi.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya huyo amewataka vijana kufika wilayani kuchangamkia fursa hizo na iwapo watakwamishwa afike ofisini kwake bila ya wasiwasi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa shina la Kawaida CCM Kata 14, Mkapaw Kafuku alisema amefarijika kuona mwenyekiti wa Vijana CCM Taifa, Mohamed Kawaida kukubali kufungua tawi hilo hivyo amemuhakikishia mwenyekiti huyo vijana wa tawi hilo wanasema mitano tena kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kawaida yupo kwenye ziara mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kufungua matawi na mashina mbalimbali ya Chama Cha Mapinduzi.
More Stories
TASHICO kutumika badala ya MSCL
Dodoma yaandaa Kongamano kutatua changamoto za ajira kwa vijana
Dkt. Pindi Chana aweka jiwe lamsingi jengo la jiolojia Karatu