Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Shinyanga
MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi amedai alilazimika kuhama katika chama chake cha awali Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa na uchapaji kazi wa Rais Dkt. John Magufuli.
Katambi ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kampeni za kunadi Sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 kwa wakazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ambao umefanyika katika Viwanja vya Ndembezi Migungani Manispaa ya Shinyanga.
Katambi amefafanua chanzo cha kudorora kwa uchumi wa wakazi wa Shinyanga ambapo amefafanua mikakati kadhaa ya kubadili hali hiyo na kwamba Jimbo la Shinyanga linahitaji watu makini ili wafanye kazi ngumu na hakuna njia ya mkato wala kutumia mapepo bali kwa kufanya kazi.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango