Fresha Kinasa, TimesMajira Online Mara.
KATIKA kuhakikisha wanafunzi wanasoma karibu na nyumbani kwao na kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu, Jimbo la Musoma Vijijini Mkoa wa Mara kupitia Mbunge wake Prof.Sospter Muhongo limeweka malengo ya kuhakikisha kila Kijiji Jimboni humo kinakuwa na shule za Msingi za kutosha pamoja na Shule ya Sekondari moja kwenye kila Kijiji.
Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 28 zenye Vijiji 68, ambapo mpaka sasa idadi ya Sekondari za kata Jimboni humo ni 26, Sekondari za Madhehebu ya Dini ni mbili, na moja ni High School,huku High School Mpya za Sayansi zikiwa ni mbili.
Hayo yameelezwa kupitia Ripoti ya ujenzi wa Sekondari Mpya Jimboni humo iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Machi 15, 2025. Ambapo pia imeeleza kuwa Sekondari Zinazojengwa na Serikali jimboni humo ni tatu,katika Vijijini vya Butata, Kasoma na Kurwaki. huku pia Sekondari zinazojengwa na wanavijiji pia zikiwa ni 3 Vijijini Muhoji, Nyasaungu na Kisiwani Rukuba.
Ripoti hiyo pia imesema Sekondari mpya zilizoanzwa kujengwa mwaka huu (2025) kwa nguvu za wanavijiji ni sita.Ambapo Chitare Sekondari, Kata ya Makojo,
Mmahare Sekondari, Kata ya Etaro, Kataryo Sekondari, Kata ya Tegeruka,
Nyabakangara, Kata ya Nyambono,
Mwigombe Tech, Kata ya Kiriba, na
Musanja Sekondari, Kata ya Musanja.
“Fedha za Mfuko wa Jimbo.Kila moja ya hizo sekondari sita tayari imepewa Saruji Mifuko 150, na nyingine zimepewa nondo” imeeleza sehemu ya Ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, Mbunge wa Jimbo ameishapiga Harambee za kutafuta vifaa vya ujenzi wa sekondari zikiwemo Chitare na kupata saruji kwa Wanakijiji mifuko 50, na Mbunge Prof. Muhongo kuchangia mifuko ya Saruji 150.
Pia,Mmahare mifuko ya saruji Wanakijiji 155, Mbunge kuchangia mifuko 155. Mwigombe Tech, mifuko ya saruji Wanakijiji 182, Mbunge Prof. Muhongo kuchangia mifuko ya Saruji 200. Na Familia Mashenene inajenga darasa.
Aidha, Mbunge wa Jimbo hilo Prof.Muhongo ameanza kutoa mifuko ya saruji ahadi zake binafsi kwa vijiji vilivyoanza ujenzi unaonekana na kufuatiliwa ipasavyo.
“Tarehe za Harambee zijazo ni
Nyabakangara Sekondari, Kijijini Nyambono tarehe 25 Machi 2025
Saa 8 mchana.Kataryo Sekondari, Kijijini Kataryo tarehe 26 Machi 2025
Saa 8 mchana na Musanja Sekondari, Kijijini Musanja tarehe 27 Machi 2025
Saa 8 mchana.
Aidha, Wanakijiji wa Kijiji cha Chitare, Kata ya Makojo wameshirikiana pamoja ambapo mpaka sasa Matofali 3,750 tayari yamefyatuliwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chitare Sekondari. Hii ni sekondari ya pili ya Kata hii ya Makojo.
Nao Wananchi wa Jimbo hilo, wameendelea kumshukuru Mbunge wao Prof. Muhongo na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Hassan kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikihusisha elimu, afya na maji.
More Stories
PAC yapongeza ujenzi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko Hanang’
Rais Samia ataka watakao kwamisha huduma za ardhi kuchukuliwa hatua
Kapinga : Ni maono ya Dkt.Samia wananchi wote wapate umeme