Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Viwege Kata ya Majohe Wilayani Ilala Amina Kapundi, awasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha 2019 mpaka 2024 .akielezea mafanikio ya Viwege aliyofanya katika kipindi cha miaka mitano.
Mwenyekiti Amina Kapundi akielezea mafanikio katika kipindi cha miaka mitano yale aliyoyafanya alisema Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kamati ya Maendeleo ya Serikali ya mtaa Viwege imetoa vyeti vya kuzaliwa 329 kwa watoto chini ya miaka mitano,pia mafanikio mengine Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam inatarajia kujenga kituo cha afya Viwege eneo la Kuvule ,Majohe ambapo ujenzi umeshaanza hatua za awali ambapo watajenga majengo ya kisasa majengo ya mahabara ,upasuaji,jengo la Mama na Mtoto ,Jengo la wagonjwa wa Nje jengo hilo la kisasa la kituo cha afya litagharimu zaidi ya milioni 500 pia ametoa Bima ya afya Bure kwa kushirikiana na Shirika la PASADA.
“Katika kipindi cha miaka mitano najivunia mafanikio mbali mbali ikiwemo nimetekeleza Ilani ya chama Mtaa wa viwege .Barabara ya Moshi Bar ,Bombambili viwege kurutini kwa sasa inajengwa mifereji na inatarajia kujengwa na Mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji( DMDP) kwa kiwango cha Lami pia Barabara Pugu Sekondari,Majohe Kivule kipande cha Halisi Sekondari kitajengwa 0.4 KM kwa kiwango cha ZEGE na itamaliziwa na Mradi wa DMDP kwa kiwango cha lami “alisema Amina.
Mwenyekiti Amina Kapundi alisema sekta ya Maji asilimia 80 wananchi wameunganishiwa maji ya salama kutoka kwa Watu Binafsi na asilimia 20 wameunganishiwa maji ya DAWASA mafanikio mengine ujenzi wa masoko ya soko la MPEMBA la mtu Binafsi na soko la Serikali mchakato wa ujenzi wake umeanza .
Aidha pia alisema mwaka 2022 amesimamia zoezi la Serikali la Anuani ya Makazi ambapo Halmashauri na Kamati ya Mtaa walipatia majina na mitaa ya Viwege zaidi ya 400 kwa sasa mitaa yote inatambulika kiserikali.
Pia wananchi wake wa viwege asilimia 99 wote wamenufaika na mradi wa REA umeme wa TANESCO ambapo ofisi ya Serikali za mitaa viwege na Wenyeviti wa Mashina walisimamia mradi huo wa kuunganisha umeme Vijijini REA kwa shilingi 27,000/=
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM mkoa Dar es Salaam Mashaka Nyasi alipongeza utendaji kazi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa viwege AMINA KAPUNDI amewataka wananchi kuunga mkono juhudi zake za kuleta maendeleo kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara viwege ya sasa ina kuwa ya kisasa.
MASHAKA Nyasi aliwataka wananchi wa Viwege Majohe kuchagua viongozi wanaotokana na ccm kwa ajili ya kuletea maendeleo kama Mwenyekiti AMINA KAPUNDI amefanya mambo makubwa ya utekelezaji wa Ilani.
“Chama cha Mapinduzi CCM ina taka viongozi wanaotumikia watu chama cha Mapinduzi kinaendelea kutumikia watu ccm itaendelea kutimiza wajibu wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi Rais wetu anaendelea kuleta maendeleo Kata ya Majohe Viwege tunaomba muahikikishe CCM inarudi madarakani “alisema Mashaka.
KATIBU wa Mbunge wa jimbo la Ukonga Hayubu Msalika alielezea baadhi ya Barabara zitakazojengwa na Serikali Jimbo la Ukonga katika mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP Banana ,Kitunda ,Kivule,Msongola,Pugu ,Viwege ,Majohe
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba