November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kapinga aeleza juhudi za Serikali kusambaza vituo vya CNG Nchini

📌 Azungumzia suala la magari ya Serikali kufungwa mfumo wa CNG

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), inajenga vituo vya kujazia gesi kwenye magari (CNG) mkoani Dar es Salaam (viwili) na mkoani Pwani (kimoja) huku TPDC ikiendelea na ununuzi wa vituo vidogo vya kujaza CNG kwenye magari vinavyohamishika ambavyo vitasimikwa katika mikoa ya Dar es Salaam (vitatu), Morogoro (kimoja) na Dodoma ( viwili).

Mhe. Judith Kapinga amesema hayo tarehe 27 Agosti, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu.

Amesema kwa sasa kuna vituo vitano vya kujazia gesi kwenye magari katika mikoa ya Dar es Salaam (Ubungo Maziwa, Tazara na Uwanja wa Ndege), Pwani (Mkuranga) na Mtwara (Dangote).

Kuhusu mpango wa magari ya Serikali kutumia mfumo wa CNG amesema kuwa tayari Mtaalam Mshauri ameshapatikana lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba suala hilo linafanyika kwa ufanisi.