Na David John Geita
MBUNGE wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu ameipongeza kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya teknolojia ya madini Kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuhakikisha maonyesho hayo yanafana na yanaleta tija Kwa wadau mbalimbali .
Amesema kuwa Maonyesho hayo yameandaliwa vizuri na washiriki ni wengi linatia hamasa, hususani ushiriki wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi umeongezeka, pia kuongezewa Kwa makampuni ya Madini hasa wanaonyesha Teknolojia ya Madini.
Kanyasu amesema Kwa mara ya kwanza Maonyesho hayo yamewaleta pamoja Watanzania wanaochimba Madini kutoka Mikoa mbalimbali nje ya nchi kuja kutangaza Biashara zao Tanzania, hivyo amewapongeza waandaaji Kwa jambo hilo kubwa na muhimu.
Pia amesema jambo pekee ambalo wananchi wanatakiwa kujua ni kwamba bado walengwa ( wachimbaji wenyewe ) ado hawajafikiwa kiasi cha kutosha.
” Ziko Kampuni ambazo lazima wawafuate wachimbaji madogo kule chini, Maonyesho haya hawawalengi makampuni makubwa kama GGM, Bakrifu, na Sota Mining, yanalenga wachimbaji wadogo kwahiyo tuangalie namna ya kuwafuata wale wachimbaji wadogo kule chini hasa kwenye kuwapeleka Teknolojia, mitaji, lakini kwenye kuwawekea bima” amesema Kanyasu.
” Kwasababu mabosi wamekuja hapa, lakini wale wachimbaji wenyewe wako kwenye mashimo, ambao hata hawajapata nafasi ya kuja kuona Maonyesho haya, na ndio wanaokufa Kwa kuangukiwa na miamba” ameongeza Mbunge Kanyasu
Ameongeza kuwa kadiri inavyoonekana Geita ilivyo sasa sivyo ilivyokua zamani, kuanzia Kasama mpaka Geita amjini palikua na msitu Mkubwa sana, lakini miti yote imekwisha kwasababu ya Uchimbaji wa madini ( Matumizi ya Matimba) ambapo amesema iko haja ya kutafuta Teknolojia itakayookoa Misitu itakayobaki ili tusiendelee kukata miti yote inayobaki tutaharibu hali ya hewa.
“Kuna uhusiano mkubwa wa hali ya hewa ya Kanda ya ziwa na Misitu ya asili iliyokuwepo, kwahiyo tuchimbe Madini tutengeneze pesa, zile pesa zirudi kupanda miti, kazi nzuri imefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii pale mbele ya Katolo ule msitu wa Bihalamulo wamepanda hekta 69,000 pale wamepanda msitu mkubwa, ifanyike hivyo kwenye maeneo yote yaliyokua na msitu wa asili lakini imevunwa kwenda kwenye madini kwaajili ya kufidia ile Misitu ambayo imeharibika, mimi nafikiri kwakufanya hivyo tutaendelea kuwa salama zaidi kwa hali hiyo” amefafanua Kanyasu.
Ameiomba Wizara ya madini kuhakikisha kwenye Maonyesho kama hayo mwakani, tuwe na Banda linaloonyesha bidhaa mbalimbali zilizokamili za mawe aina mbalimbali, maana tulipofanya Maonyesho ya Madini Dar es Salaam tulikua na watengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama mikufu, Mikanda, shanga, heleni, shanga, vitu vingi mbalimbali ambao waliletwa na Wizara.
” Sasa hapa tuna Madini yanayotupwa, kule wanaofanya uchechuaji wanakamata zaidi Dhahabu na Silva, maana Silva nyingà inabaki kwenye tope, waje na Teknolojia ya kukamata silva inayobaki kwenye tope, kwasababu sokoni tunahitaji Silva lakini sio koo kwa mchimbaji, mchimbaji anatafutwa dhahabu kwa hiyo asilimia anayopatikana baada ya kuchenjuliwa ni ile ambayo imekamatwa Kwa bahati mbaya.
Pia ameiomba Tume ya Madini kuwasaidia kuja na Teknolojia ya kuanza kukamata Silva, dhahabu, yakamatwe na Madini mengine ili tusitupe utajiri huu kwenye matope na Madini mengine kama hapa walivyokuja hapa watu wa Tanzanite kutoka Mirerani tumefurahi sana, kwasaba na Geita yapo mawe aina hii ambayo yanaweza kufanyika nakshi watu wakanunua wakavaa, wakaacha kuvaa maplastiki.
Kwaupande wake mfanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Tanzanite ya Franone Mining & Gems Company Ltd Furaha Mshai amesema ujio wao kwenye Maonyesho hayo ni fulsa pekee ya kutangaza Madini yao aina ya Tanzanite na kuwaonyesha Watanzania Madini pekee yanayopatikana hapa nchini ambayo ni Tanzania.
Mshai ameongeza kuwa Madini hayo yamekua ni kivutio kikubwa katika Maonyesho hayo yamekua ni utajiri mkubwa wa nchi ya Tanzania.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais