November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kanisa lasaidia makundi maalum

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

KANISA la New Penuel Pentecoste ,lililopo Mtaa wa videte Kidugalo Chanika Wilayani Ilala ,limetoa msaada wa vyakula na nguo kwa kituo cha kulelea watoto Yatima uhai Development Organization kwa ajili ya kusaidia watoa wa makundi maalum waweze kufurahia Krismas .

Msaada huo umetolewa na Askofu Pastory Masomhe wa Kanisa la New Penuel Pentecoste, lililopo Chanika Wilayani Ilala kwa ajili ya kusaidia watoto wa makundi maalum wa kituo hicho.

“Kanisa letu la New Penuel Pentecoste, ni utaratibu wetu kusaidia jamii kila mwaka kusaidia jamii mbali mbali waweze kufurahia wawe sawa kama jamii nyingine dhumuni la Kanisa letu kutoa msaada kwa watoto wahitaji ili wajue mahitaji yao kwani dini iliyosafi inaenda tazama yatima na mahitaji yao mpango hu bwana tesu anaupenda ” amesema Askofu Pastory

Askofu Pastory Masomhe amesema mpango huo wa kusaidia Jamii Bwana yesu anaupenda na kuwapa baraka ambapo alitoa wito kwa wadau wengine kutoa msaada katika kituo hicho cha Uhai Development Organization kilichopo Kidugalo kata ya Chanika.

Mama Askofu wa Kanisa la New Penuel Pentecoste Esther Pastory Masomhe ametoa wito Jamii nyingine kubeba jukumu la kusaidia jamii akianza na wana Ilala aliwataka wasaidie kituo hicho na kukitangaza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ameomba wakitambue .

Ether Masomhe amesema kituo hicho wamebeba jukumu kuweka jamii pamoja Taifa la kesho litatoka katika makundi maalum .

Kwa upande wake Mlezi wa Kituo hicho UHAI DEVELOPMENT ORGANIZATION Teddy Kachandwa amesema kituo hicho kina watoto 48 kituo kimeanzishwa mwaka 2012 kimesajiliwa Wilayani Temeke kina majengo manne kwa sasa wameamia Wilayani Ilala kata ya CHANIKA.

Teddy Kachandwa amesema kituo hicho kina majengo manne kwa sasa anafanya taratibu za usajili kiweze kutambulika na Serikali kwa wilaya ya Ilala .