October 9, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kanisa la sprint word Ministry lamshukuru Rais Samia

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Kanisa la Sprint word Ministry ,lililopo wilayani Ilala limetoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kutenda haki baada uchunguzi kuonyesha kanisa hilo halina hatia .

Akizungumza na waandishi wa habari Dkt.Elzabeth Kilili, mke wa Askofu Dkt Ceasar Masisi ,alisema anashukuru Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia haki na kuonekana taarifa zilizokuwa zinaichafua kanisa hilo ni za uongo .

Dkt ,Elizabeth Kilili alisema awali Kanisa hilo lilifungiwa na Serikali kutokana na kudaiwa kuchochea mapenzi ya jinsia moja baada kusambazwa kipande kidogo cha video ambacho kilisababisha taharuki.

“Tunashukuru Serikali yetu chini ya Rais Samia imetenda haki dhidi yetu uchunguzi umeisha kwamba hatuna hatia ni mtandao ya kijamii ilipotosha jamii lengo la ukweli ilionyesha sehemu ndogo ya video kutoka video kuu “alisema Elizabeth.

Dkt.Elzabeth Kilili alisema kipande hicho cha video kilikatwa na kusambazwa kutoka katika video kuu ili kuhalalisha tuhuma ambazo sasa zimezihishwa sasa ni za uongo.

Alisema Serikali ilifanya uchunguzi kama baba katika familia ,kwani Baba jukumu lake kuangalia familia na kuiokoa ambapo Serikali katika uchunguzi ilichukua hatua mbali mbali kama Baba .

Aidha alisema katika kipindi hicho cha uchunguzi Msajili alisimamisha huduma za kanisa hilo,kufunga ukumbi wa kukutania baadae kufuta usajili wa Kanisa hilo .

“Tunalishukuru Jeshi la Polisi limemaliza kufanya uchunguzi kwa kipindi cha miezi sita na kuonekana Kanisa hilo halina hatia yoyote ambapo pamoja na majibu ya jeshi la Polisi pia walipewa barua iliyowataka jengo lao la Kanisa liweze kufunguliwa na kutumika kwa shughuli za kijamii na sio huduma za kanisa “alisema.

Alisema Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni sikivu na makini tunaiomba itupe ruhusa kuendelea kuabudu Mungu hivyo wanatoa tamko hawana uhusiano wowote na wale wanaotetea mapenzi ya jinsia moja ambapo kwa sasa kanisa hilo linasubiri rufaa ambayo walikata tangu Machi mwaka huu .