Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wamezindua shule ya awali na msingi ya Jerusalem Mbezi Beach.
Maazimio ya kuanzishwa shule hiyo yametokana mkutano mkuu wa Dayosisi uliketi hivi karibu kuanza kuweka mkazo kwenye elimu, ambapo walianza ngazi ya sekondari na sasa wapo kwenye ngazi ya msingi.
Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Alex Malasusa amesema tayari shule kama hizo zimeanza katika maeneo ya Kimara hivyo wameona uhitaji mkubwa wa jamii watoto kupata elimu stahiki.
kutokana na hivyo Askofu Malasusa
amewataka wazazi kuanza kuwalea watoto kimaadili wakiwa msingi ili kusaidia kuondokana na tatizo la mmonyoko wa maadili kwenye jamii.
“Ili tuwe na jamii yenye maadili mema ni lazima maadili hayo yajengwe yakiwa msingi, maadili hayatokei tu,au huwezi kwenda kununua maadili ni lazima tushirikiane, wazazi, shule, kanisa na sisi kwa pamoja tuweze kwenda kupambana na kuporomoka kwa maadili, hivyo mimi,wewe tuungane κwenye kurudisha maadili mema kwenye jamii yetu”
Askofu Malasusa amesema, shule hiyo haifundishi tu mambo ya kielimu lakini pia watoto wanasisitizwa maadili na maisha ya kiroho hivyo aliwataka wazazi na walezi kutembelea shule hiyo ili fursa hiyo iwe kwa wote.
“Shule hii ni ya watu wote ,shule hii haina ubaguzi na hatutambagua mtu kwa rangi,dini kila mtu atapata elimu,kwani Yesu hakuja duniani kwa ajili ya watu flani alikuwa kwa watu wote”
Kwa Upande wake Mratibu wa Elimu wa Dayosisi ngazi ya pwani, Agnes Lema, amesema shule hiyo itakuwa ikitumia mtaala wa elimu ya dini kwa ajili ya kuwaleta watoto kwa maadili mema.
Lema amesema sababu ya kuanzisha shule ya Jerusalem, ni baada ya kubaini kuwepo na tatizo la mmonyoko wa maadili kwenye jamii.
“Tumeona bado kuna changamoto ya kukosa kwa maadili kwa watoto na jamii kwa ujumla,hivyo hapa tutasaidia kumlea mtoto maadili mema”
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi