Na Nasra Bkari, TimesMjira Online
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Masauni, ameitaka Benki kuu ya Tanzania kutoa leseni kwa makampuni mbalimbali yanayotoa huduma za mikopo kupitia mitandao.
Akizungumza bungeni Mkoani Dodoma jana katika kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge Tarimu, alisema, Benki kuu inapitia maombi yote ambayo yanaletwa na makampuni mbalimbali na itakapojiridhishisha itatoa leseni ka kampuni hizo.
“Makampuni mbalimbali ya simu yanatoa huduma za mikopo kupitia mitandao na riba zake zimekuwa juu sana, Je, benki kuu inafanya nini katika kuhakikisha inasimamia huduma hizi,” alihoji.
Alisema, Kampuni yoyote ikizingatia masharti kwamba lazima waambatane au washirikiane na kampuni ambayo ipo ndani ya nchi yetu basi benki kuu itatoa reseni kwa kampuni hizo.
“Benki kuu inapitia maombi yote ambayo yanaletwa na makampuni mbalimbali itakapojiridhisha itatoa leseni kwa kampuni yoyote ikizingatia masharti kwamba lazima waambatane na washirikiane” alisema Chande.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini