December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni za ndege Emirates na Air Canada zaingia makubaliano ya ushirikiano

Na Penina Malundo

KAMPUNI za ndege ya Emirates na Air Canada zimeingia makubaliano ya pamoja za ushirikiano katika kuwapa fursa wateja wao nafasi mbalimbali za kuweza kupata manufaa ya mpango wa pamoja wa uaminifu wawapo safarini.

Makubaliano hayo yalitiwa saini hivi karibuni na Makamu wa Rais
Mwandamizi wa Idara ya Emirates Skywards,
Dk Nejib Ben Khedher na Makamu wa Rais
Mwandamizi, Bidhaa, Masoko, Biashara ya Mtandaoni wa Air Canada na Rais, Aeroplan,
Mark Youssef Nasr katika
Makao Makuu ya Emirates Group huko Dubai.

Akizungumza katika makubaliano hayo,Khedher amesema watoa huduma hao waliamua kuanzisha ushirikiano huo wa kushiriki kwa lengo la kuwapa
wateja muunganisho katika Bara la Amerika Kaskazini, Asia, Mashariki ya Kati
na Afrika.

“Wateja wa Emirates sasa wanaweza kuhifadhi safari za ndege kwenda au kutoka maeneo ya Kanada hususani katika eneo la Toronto, ikijumuisha Calgary, Edmonton, Halifax, Montreal, Ottawa na
Vancouver,”amesema na kuongeza

“Tunafuraha sana kwa kuimarisha ushirikiano wetu na Air Canada
na kuanzisha rasmi toleo letu la pamoja la uaminifu kwa pamoja, karibu wateja milioni 40 wanaosafiri wataweza kusafiri kwa mtandao wa pamoja wa zaidi ya maeneo 350 na kufurahia huduma waliyochagua,”amesema

Amesema wanatarajia kufungua fursa nyingine kwa wateja wao waaminifu na pia
kuwakaribisha wateja wa Aeroplan ndani ya Emirates na kuwaonyesha bidhaa zao zilizoshinda tuzo na
huduma za kipekee.

Kwa upande wake, Nasr, amesema programu hizo mbili za makubaliano ni uaminifu
unaotambulika zaidi katika maeneo yao na zinakuja pamoja ili kutoa kitu kizuri katika usafiri wao was kutumia ndege hizo.

Amesema fursa hii itaweza kuunganisha marafiki na familia kutoka kwa watu wa Kanada na nchi nyingine na kusaidia wasafiri kuona baadhi ya maeneo yanayosisimua zaidi duniani.

“Tunajivunia kushirikiana na Emirates na Skywards huku Aeroplan ikiendelea kutimiza ahadi za Wateja wake kusafiri vizuri zaidi,makubaliano hayo mapya yatawawezesha wanachama wa Emirates Skywards kupata ya kutembea na kufanya safari zote za ndege za Air Canada zinazostahiki,”amesema