December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania yatoa mafunzo kwa waandishi

Na Esther Macha, Timesmajira,Online,Mbeya

SERIKALI mkoani Mbeya imesema kuwa kuna jitihada kupitia Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC),kuzalisha Megawati 200 za umeme na Megawati 500 za joto kufikia 2025 .

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Mkoa wa Mbeya,Festo Sikagonamo

Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ,Mariam Mtunguja wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari 27 wa Mikoa ya Songwe na Mbeya kuhusu Tansia ya Nishati ya Jotoardhi nchini yaliyoandaliwa na Kampuni ya uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC).

Mtunguja amesema kuwa kufikia mwaka 2025 watakuwa wamezalisha Megawati 200 za umeme na Megawati 500 za joto ambazo zitatokana na miradi ya kipaumbele ya ngozi na Kiejo Mbaka-mkoani Mbeya,Songwe,na Mkoa wa SOngwe,Luhoi Mkoa wa Pwani na Natron Mkoani Arusha.

“Ndugu zangu waandishi wa habari nimeelezwa kuwa baada ya mafunzo haya mtatembelea eneo la mradi wa Jotoardhi Mbaka Kiejo ulioko Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe tumieni fursa hiyo kuelewa kwa vitendo zaidi namna ya nishati hiyo inavyotafutwa kisayansi”amesema Katibu Tawala.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya,Mariam Mtunguja akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya na Songwe

Aidha Mtunguja amefafanua kuwa katika eneo hilo kuna mradi unaoendelea kutekelezwa wa uchoraji visima vya utafiti wa rasilimali ya Jotoardhi.

Hata hivyo Katibu Tawala huyo ametoa wito kwa waandishi wa habari kutumia fursa hiyo muhimu kutola na uelewa wa kutosha wa nishati ya jotoardhi na kusema kuwa mafunzo hayo yatasaidia waandishi wa habari kuwae na usahihi wakati wa kutoa taarifa zinazohusu nishati ya jotoardhi na kufanya umma wa watanzania kupata taarifa zenye usahihi zaidi .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya ,Festo Sikagonamo ameshukuru kampuni ya uendelezaji Jotoardhi Tanzania kwa kuleta mafunzo hayo kwa waandishi wa habari.

Sikagonamo amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja kwa muda mwafaka kwa waandishi wa habari kwani yamefungua mlango.