January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Heritage Drinking Water yazindua mashine ya maji, kituo cha mwendokasi Kimara

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Kampuni ya kitanzania Heritage Drinking water LTD imeendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutunza na kuboresha mazingira kwa kutoa huduma ya maji safi kwa watanzania yanayopatikana katika chupa ambayo mwananchi akiitumia hatoweza kuitupa na kupeleka kuchafua mazingira.

Huduma hiyo imeenda sambamba na ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kuongeza ajira kwa vijana nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya maji safi kutoka kampuni hiyo ya Heritage Drinking water uliofanyika katika kituo cha mwendokasi Kimara mwisho, leo jijini Dar es Salaam, Mbunge wa jimbo la kibamba Issa Mtemvu alisema hadi sasa huduma hiyo imefika katika vituo 20 na kuendelea na utoaji wa huduma ya maji safi.

“Miaka ya nyuma Serikali iliweka jitihada mbalimbali za kuondokana na uchafuzi wa mazingira kupitia mifuko ya plastiki ambapo tukaona kuna plastiki nyingine ambazo zinaleta madhara sana hivyo kupitia heritage drinking water mazingira yanakua salama”

“Pia huduma hii inaongeza ajira ya vijana ambapo wameajiri vijana 60 wakienda sambamba na ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kwamba ndani ya miaka mitano tuweze kuajiri watanzania milioni nane” Alisema Mtemvu.

Mtemvu alisema asilimia 75 ya miili ya binadamu hivyo Heritage Drinking water wamewarahusishia wananchi wake kwa kuwapatia maji kwa bei nafuu.

“Kupitia huduma hii, watanzania wanapata fursa ya kunywa maji kwa bei ndogo sana ambapo ni shilingi 200 kwa lita moja”

Mtemvu alimshukuru Mkurugenzi mtendaji na uongozi mzima wa kampuni ya Heritage Drinking water kwa wazo hilo na uwekezaji huo ambao wanaendelea nao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dkt. Edwinus Lyaya alisema huduma hiyo imeanza leo siku ya uzinduzi na itakua ni endelevu kuanzia asubuhi, mchana na usiku.

“Lengo la kufungua kituo hiki ndani ya kituo cha mwendokasi ni kuhakikisha kwamba tunatoa huduma kwa wasafiri wanaotumia mwendokasi kwasababu maeneo haya yalikua hayana huduma hii muhimu ya maji ya kunywa”

“Tumeona tuweke huduma hii ya mwendokasi ili wasafiri wanaokua na kiu waweze kunywa maji, wasafiri wakiwa na heritage water”

Naye abiria wa kituo cha mwendokasi kilichopo Kimara, Elizabeth Robert alisema maji hayo ni mazuri na ni salama pia ni bei rahisi na unajipatia chupa ambayo utaendelea kuitumia kwa matumizi mengine hapo baadae.

Mteja mwingine ambaye amepata huduma hiyo ya maji katika kituo cha mwendokasi kimara, Abdurahman Hamisi alisema huduma ni nzuri na wameipokea kwani inawasaidia watanzania kwa kupata maji ya bei rahisi, itamsaidia kuweka akiba ya pesa.

“Tunamshukuru Mbunge wetu kwakuwa yeye ndiye amesababisha kusukuma kwa kiasi kikubwa mpaka huduma hii imefika mahali hapa, hivyo kama kuna wengine hawajapata huduma hii wakaribie kupata huduma ya maji kwasababu ni mazuri na unapata faida ya chupa”

Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu ( kulia ) akikata utepe akizindua rasmi huduma ya maji safi na salama ya Heritage Drinking Water katika kituo cha Magari ya Mwendokasi Kimara Mwisho leo Jijini Dar Es Salaam , Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dkt. Edwinus Lyaya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Heritage Drinking water Dkt. Edwinus lyaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya maji safi na salama ya Heritage Drinking Water katika kituo cha Magari ya Mwendokasi Kimara Mwisho leo Jijini Dar Es Salaam , Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dkt. Edwinus Lyaya.
Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu ( kulia ) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya maji safi na salama ya Heritage Drinking Water katika kituo cha Magari ya Mwendokasi Kimara Mwisho leo Jijini Dar Es Salaam .
Baadhi ya abiria katika kituo cha mwendokasi Kimara Mwisho wakipata huduma ya maji safi kutoka kampuni ya Heritage Drinking water leo Jijini Dar es Salaam.