November 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya GF yaiomba serikali kuiunga mkono Hyundai Kuwezesha kutengenezwa nchini

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wakati wa maonyesho ya biashara ya kimataifa yakifunguliwa na mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan walitembelea mabanda mbalimbali kabla ya kufungua na kutoa zawadi kwa washindi mbali mbali.

Akizungumza wakati Marais hao wakitembelea banda lao Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd , Imrani Karmali amesema baada ya ziara ya Rais nchini Korea
kushawishi wawekezaji kuwekeza nchini wao kama GF Automobile, wamezungumza na wakorea na wako tayari kuja kuweka kiwanda cha kuunganisha magari ya Hyundai nchini.

Amesema wakorea hao walitaka lazima kuwe na oda kubwa kwa kuanzia sasa ambapo wao kupitia kiwanda chao cha kunganishia magari cha GFA wapo tayari kufanya hivyo.

“Ombi letu kwako mama tunaomba Serikali kupitia wizara na tasisi zake kutuunga mkono katika hili na matunda ya ziara yako nchini korea kuonekana kwa Hyundani kutengenezwa nchini Tanzania”

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi wakizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd, Imrani Karmali wakati walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa sabasaba leo Jijini Dar es Salaam (Picha na Mpigapicha wetu)