Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Wentworth Gas Ltd, Katherine Roe amesema kutokana na ufanisi mkubwa wa kifedha kampuni hiyo inazalisha gesi ili kuivusha Tanzania katika uchumi wa kesho.
Roe amesema hayo leo Agosti 4,2022 wakati akizindua ripoti ya mipango endelevu ya mwaka 2021 ya kampuni hiyo ambayo inachangia ripoti kuu ya Kampuni ya Wentworth Resources Plc.
Amesema kampuni hiyo inashirikiana na Serikali ya Tanzania kuunga mkono agenda yake ya maendeleo ya Taifa katika nishati na mazingira, ambapo kwa kufanya hivyo wameboresha maisha ya watu.
Pia, amesema kampuni hiyo inachangia mageuzi ya nishati nchini kwa kuwezesha umeme wa bei nafuu pamoja bna uwekezaji katika miradi ya elimu, afya na maendeleo ya kiutamaduni.
“Kwa kusambaza gesi asilia yenye kiwango cha chini cha kaboni nchini ni kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na matumizi ya viwandani,”amesema Roe
Aidha, Mkurugenzi huyo, amesema ripoti hiyo inatoa maelezo zaidi kuhusu utendaji wa masuala muhimu ya mazingira, kijamii, na Utawala wa mwaka mzima.
Roe amesema ripoti hiyo pia inaelezea mtazamo wa Wentworth kupitia mkakati endelevu unaowiana na malengo ya maendeleo endelevu ya Kiamataifa inayozingatia nguzo tano za kimkakati.
“Nguzo hizi ni kusaidia mpito wa nishati unaowajibika, kuwezesha mabadiliko ya nishati,kujenga nguvu kazi mbalimbali, kuendeleza ukuaji kupitia ushirikiano pamoja na Utawala wa mazingira, kijamii na utawala,”amesema Roe
Pia, amesema kampuni hiyo inaendelea kupunguza uzalishaji wake kaboni baada ya kupata mojawapo ya viwango vya chini vya kaboni kwa mlingano wa kila pipa la mafuta katika sekta ya mafuta na gesi.
Kwa upande wake, Meneja Ushirika wa Wentworth Gas Ltd, Khalifa Ngaga amesema kwa kipindi chote hadi ripoti yao inazinduliwa wamefanya kazi bila kusimamisha miradi yoyote wala hakuna majanga ambayo yametokea katika shughuli zao ambayo yangefanya kazi isimame.
Amesema, kutokana na ahadi ya Serikali kwamba kufikia 2030 itakuwa imepunguza kwa asilimia 30 hewa ya ukaa, wanatarajia kuanzisha programu za kuzalisha vitu vitakavyopunguza athari hapa nchini.
“Tunafikiria kuanzisha majiko yanayotumia kuni chache, mradi huu utaweza kusaidia watu kupika kwa kutumia kuni tano au mbili kuivisha chakula chao na zaidi hapo tutaanzisha mradi wa kuchuja maji,”
“Hii miradi yote miwili itahusika katika maeneo ya vijijini ambayo kwa njia moja au nyingine wananchi hawezi kumudu kununua maji na kuchemsha,”amesema Ngaga
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano