December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Champion Rise yaandaa tuzo za waogeleaji

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Champion Rise inatarajia kutoa tuzo za mchezo wa kuogelea hapa nchini ambazo zinatarajia kufanyika Dicember 19 mwaka huu.

Katika tuzo hizo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Amina mfaume amesema hii ni mara ya pili kuandaa kwa tuzo hizo na lengo la kutolewa kwa tuzo hizo ni kuongeza hamasa za mchezo wa kuogelea kwa wachezaji na wadau wa mchezo huo.

“Hii ni mara ya pili kuandaa tuzo hizi lengo kubwa ni kuona mchezo wa kuogelea unazidi kukuwa, hivyo kutokana na hamasa kuwa ndogo kwa watanzania tunaamini tuzo hizi zitatusaidia tuzidi kuhimiza watanzania, washikamkono na watu wanaoupenda mchezo huu ili kuweza kusaidia”

Amesema kuwa, katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo, kutakua na vipengele mbalimbali ikiwemo kipengele cha muogeleaji wa mwaka, muogeleaji chipukizi wa mwaka na meneje wa club wa mwaka.

” Kwa mwaka huu tuzo zitafanyika katika hotel ya Hyatt Regency siku ya jumapili ambapo utoaji wa tuzo hizi utakua endelevu “amesema Amina.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni hiyo Ally Nchahara, amesema viingilio katika sherehe hizo ni shill laki moja kwa mtu mmoja, shilingi mill 1.5 kwa meza na shilingu mill moja kwa VIP huku akiwataka wadau wa chezo wa kuogelea kujitokeza kwa wingi.

“Tunawaomba wadau mbalimbali wa mchezo wa kuogelea yakiwemo makampuni na vilabu kujitokeza kwa wingi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo ili kuheshimisha mchezo wa kuogelea hapa nchi”amesema Nchahara