Na Penina Malundo,Timesmajira
MKURUGENZI wa Kampeni ya Wewe ni wa Thamani Aziza Suedi amesema wanatarajia kuzindua kampeni hiyo hivi karibuni kwa lengo la kurudisha imani kwenye miyoyo ya vijana kutokana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo na kuwasababisha waweze kukataa tamaa.
Akizungumza na Mwandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,amesema Kampeni hiyo inaendeshwa na vijana wa Kitanzania ambao wameshuhudia vijana wengi wakiwa wanaingia katika makundi mabaya mbali mbali ambapo inapelekea kujihusisha na madawa ya kulevya, Utumiaji wa pombe kali na kujiunga makundi mengine yasio na faida kwao wala kwa jamii.
Amesema kampeni hiyo imejikita katika kumsaidia kijana wa kitanzania kuijuia thamani yake na kujua mchango wake kwenye jamii na taifa kwa ujumla.
“Natoa wito kwa wadau wa maendeleo wote nchini kuungana nao katika harakati za kumtengenezea kijana mazingira mazuri ili awe faida kwao na jamii inayowazunguka ,”amesema.
Aidha amesema kampeni hiyo ni ya nchi nzima hivyo itakuwa ya awamu kwa awamu ambapo itaweza kuwafikia vijana wengi zaidi.
“Kampeni hii tunatarajia kuzindua mwezi ujao ambapo tunaamini vijana watabadilika na kuchukua hatua stahiki za kuwasaidia kutimiza ndoto zao,”amesema.
More Stories
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake