Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Kampeni ya Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, kutoa taulo za kike kwa shule za Sekondari Jimbo la Segerea zimeshika kasi ambapo Wanafunzi wa shule sita wamefanikiwa kupewa taulo za kike.
Kampeni hiyo endelevu imeendelea Jimbo la SEGEREA jana ambapo Msaidizi wa Mbunge Lutta Rucharaba, alifanikiwa kutoa (Pedi ) kwa shule za Sekondari za Kinyerezi,Bonyokwa,Magoza,na Kinyerezi mpya tukio hilo lilifaniyika katika shule ya Kinyerezi Anex Wilaya llala
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi taulo hizo Katibu wa Mbunge Lutta Rucharaba, alisema kampeni hiyo ya Mbunge kuwawezesha watoto wa kike wazingatie masomo ni endelevu ambapo taulo hizo za shule nne zilizotolewa na wadau wa Elimu shule ya Fountain Gate Princess iliyopo Segerea na kufikisha jumla ya shule sita kati ya Sekondari 16 zilizopo jimbo la Segerea.
“Ofisi ya mbunge wa Jimbo la SEGEREA imekuwa ikifanya kazi za Mbunge kila siku kuratibu na kusimamia kwa sasa Mbunge yupo Dodoma katika Kikao cha Bajeti huku kazi zake zinaendelea jimboni nimemwakirisha kukabidhi taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wetu waweze kujiamini wawapo darasani”alisema Rucharaba
Lutta Rucharaba alisema Wanafunzi wa kike wanakuwa watoro wanapofika Siku ya mzunguko wao wa mwezi wanashindwa kuhudhuria masomo Mbunge wa Jimbo la Segerea amendelea na Kampeni yake ya kugawa taulo akiwataka wazingatie masomo na kukuza taaluma Ili waweze kuongeza ufaulu darasani.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Kinyerezi mpya Happiness Pallangyo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli kwa kuendeleza kampeni yake ya kuwajali watoto wa kike waweze kushiriki masomo kukamilifu.
Mkuu Pallangyo alisema kitaaluma Sekondari ya Kinyerezi Mpya kila mwaka inafanya vizuri katika ufaulu shule mwaka jana 2021 Wanafunzi wawili wameferi matokeo ya kidato Cha pili , mwaka huu ndio kidato Cha nne Cha kwanza.
Alitumia nafasi hiyo kuwaomba Fountain Gate Msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya shule yao ya Kinyerezi Mpya.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Princess Augustino Fulgence alisema wanaunga mkono juhudi za Mbunge wa Jimbo la SEGEREA Bonah Ladslaus Kamoli kwa kuwajali watoto wa kike kwa ajili ya kuwajengea Mazingira Bora ya Elimu wawapo darasani.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi