January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamishina wa Dawa za Kulevya aleza jitihada za serikali mapambano dhidi ya dawa za kulevya

N a Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

KAMISHNA wa Kinga na Tiba Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini Dkt. Peter Mfisi amesema Moja ya majukumu yanayofanyika na Mamlaka hiyo ni kutoa Elimu kuhusu mapambano dhidi ya dawa za Kulevya kwa watumiaji Ili waachane na matumizi ya dawa hizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga kutembelea Banda la Mamlaka hiyo katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

“Katika nchi yetu Kuna vijana wanaotumia dawa za Kulevya za Sina mbalimbali ,lakini sisi licha ya kukamata lakini tunekuwa tukitoa Elimu kwa watumiaji waachane na matumizi ya hizo wasiendelee kupotea.

Aidha amesema kutokana na jukumu hilo wameweza kuokoa vijana wengi ambao wamejiepisha na matumizi ya dawa hizo.

“Hata hapa katika viwanja vya Nane Nane tupo kwa ajili ya kuelimisha jamii maana   dawa za kulevya pia zipo  nchini kwetu za aina mbalimbali na zinaathiri vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa.”amesema Mfisi

“Lakini pia zipo dawa aina mbili  za kulevya zinazotengenezwa viwandani kama heroin, kokein na dawa zingine lakini kuna dawa zingine zinatokana na kilimo kama bangi, Mirungi kwa hiyo ushiriki wetu Nane Nane  ni juu ya kuwaelezea wakulima kwamba wakati mwingine wasijihusishe na mazao hayo haramu kama bangi na mirungi.

Amesema wapo baadhi ya wananchi wanalima mashamba makubwa ya bangi ambao pia tunekuwa tukiwaelimisha kuhusu kuachana na kilimo hicho na badala yake wajiingize kwenye kilimo Cha mazao ya chakula yanayoweza kukuza uchumi wao.

”Hapa tunatoa elimu ya jumla juu ya madhara ya dawa za kulevya kwa sababu ukiangalia tangu tumeanza maonesho watu waliopita kwenye banda letu ni wengi sana wanafika 10,000 kwa hiyo idadi hiyo wamekuwa na uelewa kuhusu madhara yanayotokana na dawa za kulevya,” amesema Mfisi.

Pia kiongozi huyo amesema kuwa moja ya mikakati ya mamlaka kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ni kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara yanayotokana na madawa ya kulevya ili jamii ijijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya.