Na Sophia Fundi, Timesmajira Online, Karatu
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Karatu, wamekutana na uongozi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kujadili changamoto kutokana na wanyama wanaovamia makazi ya wananchi walioko pembezoni mwa msitu wa hifadhi wilayani humo.
Katika majadiliano hayo pande zote zimekubaliana kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na wanyama hao ambapo wamepanga kutoa elimu hasa kwa wananchi jinsi ya kukabiliana nao.
Mbali na elimu, pia wameweka mikakati ya kuweka uzio maeneo ambayo yameathirika pamoja na kuweka mizinga ya nyuki ili kuwafukuza wanyama kama Tembo ambao wamekuwa wakiwajeruhi wananchi na kuwaua pamoja na kuharibu mazao yao.
Akizungumza katika mjadala huo, Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Elibariki Bajuta amesema mamlaka imejipanga kuweka uzio kilometa 30, katika maeneo yaliyoathiriwa na wanyama kuhakikisha wananchi walioko pembezoni mwa msitu wanakuwa huru kufanya shughuli zao za kijamii.
Hata hivyo amesema, watashirikiana na halmashauri ya wilaya ya Karatu kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kuhakikisha maeneo yote yanapata ulinzi wa kutosha kuwazuia wanyama wakali ambao wanatoka msituni,
Pia katika mjadala huo pande hizo mbili zilijadili ni kwa namna gani wanaboresha huduma kwa wageni (watalii) kutokana na idadi kubwa kuingia nchini katika kipindi hichi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dadi Kolimba amesema asilimia 80 ya wageni wanaoigia ndani ya Kreta na Serengeti wanapitia Katika wilaya hiyo hivyo ni fursa kwa wadau wa utalii na wananchi kuwekeza wilayani hapo.
Amewataka wadau wa utalii kwenye Hoteli zao kuboresha huduma ikiwemo kuongeza vitanda kwani kutokana na filamu ya Rayol Tower aliyotagaza Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluh Hasan wanategemea kuwa na wageni wengi Sana.
“Katika kipindi hichi wageni watakuwa wengi Sana naomba wawekezaji waje kuwekeza Karatu na walio na mahoteli waongeze huduma ikiwemo vitanda vya kutosha,”amesema Kolimba.
%%%%%%%%%%%%%
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi