September 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya kudumu ya Bunge yaipongeza UDSM

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imesema hatua ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ya kufanya mapitio ya mitalaa ili kukidhi matakwa ya soko la ajira yameweza kuisadia nchi kuondokana na tatizo la ukosefu wa Ajira


Hayo yalibainishwa Agosti 10,2024 Jijini Dar es  Salaam na kamati hiyo wakati imefanya Ziara kwenye chuo hicho ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET).

Mratibu wa mradi huo, Profesa Benardera Killian alisema tayari chuo hicho kimefanya mapitio ya mitalaa 60 kwa ngazi ya shahada ya kwanza na ya pili na iko katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kutumika.

“Pamoja na kujenga kampasi mpya na kufanya upanuzi wa zilizopo tumefanya pia mapitio ya mitalaa ili iendane na soko la ajira. Tumewapitia waajiri 4,000 wametoa mapendekezo yao nini kifanyike ili kupata wahitimu bora na tumeyafanyia kazi.

“Tumeshaipeleka mitaala iangaliwe na wizara ya elimu na wao wametoa mapendekezo yao tunayafanyia kazi kabla ya kuipeleka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ili kupata ithibati kisha ianze kutumika,” amesema Profesa Benardeta.



Mwenyekiti wa kamati hiyo, Husna Shekiboko alisema kwa muda mrefu ajira imekuwa kilio cha vijana licha ya kusoma elimu ya juu, hivyo tathmini ya aina hiyo ni muhimu ili kuhakikisha elimu inayotolewa ndiyo inahitajika kwenye soko la ajira.

“Kilichofanyika ni kizuri maana tusijifungie kwenye kutoa elimu bila kujifanyia tathmini kujua elimu inayotolewa inatatua changamoto zinazotuzunguka? Je mhitimu kwa ngazi ya chuo kikuu ana uwezo wa kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.

“Tumefurahishwa pia na taarifa kwamba mnafanya tafiti ila tunachotaka matokeo ya tafiti hizi yawekewe wazo ili ziwe msaada kwenye jamii isiwe tafiti zinafanyika na kuishia kwenye makabati,” alisema Husna.

“Tumefurahishwa pia na taarifa kwamba mnafanya tafiti ila tunachotaka matokeo ya tafiti hizi yawekewe wazo ili ziwe msaada kwenye jamii isiwe tafiti zinafanyika na kuishia kwenye makabati,” aliongeza Husna.

Kuhusu jengo hilo la utawala na taaluma Profesa Killian alisema litahusisha madarasa manne yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 216, ukumbi wa mikutano wa watu 150 na maabara tano.

Alisema taasisi hiyo kwa sasa inadahili wanafunzi 88 ila ujenzi utakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 200.

“Sisi kama watunga sera tungependa kusikia kutoka kwa wataalamu mtueleze shida ni nini na tunawezaje kukabiliana na hiki kilio cha ukosefu wa ajira kwa vijana wengi,” alisema Sima.

Profesa Killian alisema kwa upande wa Taasisi ya Sayansi za Bahari inagharimu Sh11.1 bilioni ukihusisha ujenzi bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40, jengo la utawala na taaluma Mbunge wa Singida Mjini, Musa Sima amesema suala la mapitio ya mitalaa linapaswa kufanyiwa kazi na vyuo vyote na Serikali kuyafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wataalamu.

“Naamini hadi chuo kikuu kimeamua kufanya mapitio ya mitalaa ni lazima kimefanya utafiti na kuona kuna changamoto, ni vyema ingeweka wazi mmeona nini isije kuwa hatua zinachukuliwa ngazi ya juu kumbe tatizo limeanzia chini.