Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira leo tarehe 15 Februari, 2022 imefanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambapo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.David Kihenzile(MB) amewaongoza wajumbe wa Kamati hiyo katika kupokea Taarifa ya Utekelezaji ya majukumu ya TanTrade na kukagua miundombinu ya Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J K. Nyerere (sabasaba)
Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati Mhe. David Kihenzile (MB) ameupongeza uongozi wa TanTrade kwa jitihada unazofanya katika kusimamia biashara nchini na hasa namna walivyoweza kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Dunia ya Expo2020 Dubai. Kupitia maonesho hayo , Tanzania ilifanikiwa kusaini jumla ya Mikataba 36 yenye thamani ya Shilingi Trilioni 17.35 ambayo utiaji wa saini wa mikataba hiyo ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati Kongamano la Biashara liliandaliwa tarehe 27 Februari baada kusherekea siku ya Kitaifa ya Tanzania tarehe 26 Februari 2022.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe(MB) ambaye aliongozana na Kamati, aliwapongeza Wajumbe wa Kamati hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yao ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho ya Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K Nyerere (SabaSaba)ili kuwa na miundombinu ya kisasa na kuweza kuwavutia wafanyabiashara wengi zaidi kutoka ndani na nje kujitangaza.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi.Latifa Mohamed Khamis akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya TanTrade kwa Kamati hiyo amesema mpaka kufikia mwezi Februari, 2022 TanTrade imefanikiwa kupata Soko la nyama nchini Qatar kiasi cha tani 120 za nyama za mbuzi, Saudi Arabia tani 100 za nyama ya ng’ombe kwa mwezi pamoja na kuwakutanisha wazalishaji wa nafaka, muhogo, soya, asali, viungo, bidhaa za ngozi, chai na kahawa kuweza kuyafikia masoko ya nje ya nchi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi