January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya Bunge yaishauri Wizara ya Maliasili

Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online

Wizara ya Maliasili na Utalii imeshauriwa iendelee kuisimamia vyema miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo ya hifadhi ili miradi hiyo iendelee kuchangia zaidi katika uchumi wa nchi na kuboresha huduma za utalii nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti,Daniel Sillo baada ya Kamati hiyo kuhitimisha ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Wizara katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Sillo amesema Kamati yake imeridhishwa na ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali mara baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Wizara hiyo inayotekelezwa kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Waziri wa Maliasili na Utalii akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Bunge ya Bajeti.

” Ubora wa miradi tuliouona umetupa picha nzuri ya nidhamu kubwa iliyo kwenye Jeshi letu la Uhifadhi, miradi hii inatekelezwa kwa wakati na thamani yake inaendana na fedha mlizopewa, hakikisheni mnaendeleza kasi hii. Amesisitiza Sillo.

Akiishukuru Kamati hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara anayoiongoza itaendelea kuufanyia kazi ushauri na kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na
Kamati wakati wa ziara wakati wa ziara hiyo kwa kuisimamia vyema na kuhakikisha inatoa mchango uliokusudiwa katika kuimarisha uhifadhi na kuendeleza Utalii hapa nchini.